Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

IJUE ZAIDI DAWA TA TRUVADA LEO.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Yapo matumaini makubwa ya kukabiliana na janga la Ukimwi kama wananchi watakubali kuwa mstari wa mbele kupambana na adui huyo mkubwa anayeingia nyumbani.

Mbinu nzuri ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi na ambayo haina madhara ni kubadili tabia kwa kutokushiriki ngono zembe na kuwa na mpenzi mmoja.Taarifa tulizonazo mpaka sasa ni kuwa bado haijapatikana dawa au chanjo ya Ukimwi ingawa watafiti na wanasayansi wanafanya jitihada kubwa kutafuta au kuvumbua dawa ya kutokomeza kabisa virusi vya Ukimwi duniani kwa sababu vinasababisha magonjwa anuai.

Mpaka hivi sasa wataalamu wa tiba wamefanikiwa kuvumbua dawa ya kuvidumaza virusi vinapoingia mwilini, hivyo ndiyo kusema kuwa dawa ya kuviua kabisa bado haijapatikana.Ipo dawa inayotumiwa maalumu kwa ajili ya kuwakinga watu waliofikwa na masaibu ya kubakwa ili wasipate maambukizi ya Ukimwi, dawa hii inaitwa Truvada, ambayo ni mchanganyiko wa dawa mbili; Tenovofir na Emtricitabine. 

Dawa hii imethibitishwa kuwa salama kwa kupunguza makali ya VVU, lakini hutumika kama kinga katika hali maalumu tu. Hivi sasa kumeibuka mambo ya kutisha; wale wanaofanya biashara ya ngono wamekuwa wakitumia dawa ya Truvada ili kujikinga na maambukizi ya Ukimwi au kujizuia wasiambukize wengine.

Hata kama ni kweli dawa hiyo kwa kiasi fulani ina uwezo wa kinga, lakini ni wazi kuwa si dawa ya kutumiwa kila mara na watu ambao bado hawajapata maambukizi labda kwa wale tu wanaobakwa, lakini kuifanya kama ndiyo njia mbadala ya kujikinga na Ukimwi si sawa. 

Dawa za kufubaza virusi (ARV’s) kwa kawaida hutolewa bure kwa wale walioambukizwa na ambao wako katika programu ya kutumia dawa tayari, hivyo matumizi haya ya Truvada kiholela, si matumizi yanayotambulika kisheria.Hiyo maana yake ni kwamba; 

wakati Serikali inatumia mamilioni ya fedha kununulia dawa za kuwarefushia maisha raia wake waliopata maambukizi ya virusi kwa bahati mbaya, wapo wanaozifanyia mchezo dawa hizi, kwa raha zao tu, bila kujali wala kutumia kinga wanaamua kutumia dawa zilizoagizwa kwa ajili ya wale wanaozihitaji kutokana na matatizo waliyonayo, wanatokea watu wanaoelekeza matumizi ya dawa hizi kwa mahitaji mengine, ambayo kimsingi wana matatizo ambayo wanaweza kuyaepuka kwa kutumia mipira ya kiume/kike au kuacha kufanya ngono kiholela.

Wakati umefika kwa wanaodhibiti dawa hizi kulivalia njuga suala hili. Wakomeshe matumizi ya dawa za Truvada kwa matatizo yasiyokusudiwa, kwani hali hii inaweza kusababisha kuadimika kwa dawa hizo muhimu kwa watu wenye virusi na pia kufungua milango ya soko haramu kwa dawa hizo, kwa sababu bila shaka mahitaji yakizidi dawa hizo zitauzwa kinyemela tena kwa bei mbaya.

Ingawa wapo madaktari wanaothibitisha kuwa dawa ya Truvada inazuia mtu kupata maambukizi ya Ukimwi, lakini kiukweli ni kuwa dawa hiyo bado haijathibitishwa kutumika kwa mustakabali huo, hivyo wananchi wanapaswa wawe na subira kabla ya kuhalalisha matumizi ya dawa hizo kama mbadala wa mipira ya kiume.

Sote tunafahamu kuwa kinga ni bora kuliko tiba, kwa hili la Truvada kutumika kama kinga, bado wakati wake, tusubiri hadi itangazwe rasmi, tusigeuke madaktari wenyewe.

Hakuna dawa yenye faida tupu bila madhara, hivyo tunashauri kuwa wataalamu wa tiba wafanye utafiti wa kina kuhusu madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya dawa hii kiholela bila ushauri wa daktari na kama kweli dawa hii ni kinga, itangazwe hivyo na watu waitumie kama kinga ya ugonjwa wa Ukimwi. Wananchi wanataka kujua ukweli kuhusu suala hili.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top