Hizi ni picha ambazo zinaonesha jinsi mtaa wa Watanzania ulivyovamiwa, na watu kupigwa sana huko nchini South Africa siku ya jana.
Afrika Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika ambao umevutia Waafrika wengi kukimbilia huko kwa ajili ya kufanya
kazi kama za Udereva, uuzaji mafuta
kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi
nyingine mbalimbali za kijamii nchini hapo.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni
kwamba Watanzania ambao wanamiliki na
kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za
Maduka na wale wanaomiliki hoteli,
wamevamiwa wakiwa kwenye mali zao na
kufanyiwa uharibifu na nyingine kuchomwa moto.
Ni kundi la watu ambalo linaendeleza
uvamizi huu ambapo linawashutumu
Watanzania hawa kuhusika na biashara ya
dawa za kulevya, yani kwa ufupi Watanzania wanasema hata kama kweli wangekua wanafanya hii biashara, walio na mamlaka ya kuwavamia ni Polisi na sio hao raia wa kawaida.
Inaaminika kuwa kundi hili lina sehemu kubwa
ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo
ambao wamekua wakiumizwa na jitihada
za raia wa kigeni wa Nigeria na Watanzania
ambao wamejazana kwenye mtaa wao
wakimiliki maduka mbalimbali yakiwemo
ya nguo, vipodozi pamoja na hoteli.
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na
Watanzania hao na kuahidi kulifatilia jambo hilo kwa ukaribu zaidi na kubaini chanzo cha tatizo hilo. Katika tukio hilo ni Watanzania watano ambao wamejeruhiwa na watatu bado wako hospitali na mmoja kati yao kavunjika mkono, na mmoja kapigwa akiwa amepigwa sana sehemu ya kichwani.
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi
kufunga maduka yao, maduka matatu ya
Watanzania pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na Watanzania zilivamiwa
na watu wote walichuchukuliwa simu zao, huku watu wakiendelea kupigika sana.
Baada ya mda mfupi polisi walipokuja hakuna
chochote kilichofanyika zaidi ya kuchukua maelezo kwa wahanga wa tukio hao kisha kuondoka zao katika maeneo yao ya kazi.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania
akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa
kufunga duka lake na kuweza kujinusuru.



