Ikiwa leo Aprili 7, 2014 ni miaka miwili imepita tangu msanii mahiri wa filamu bongo Steven Kanumba afariki dunia, wasanii mbalimbali hapa nchini wameandika ujumbe wa kumuenzi huku wengine wakiandika maneno ya huzuni na jinsi wanavyomkumbuka Kanumba
Miongoni mwa wasanii hao ni Swebe, Wema Sepetu, Flora Mvungi, Aunt Ezekiel na wengine wengi katika kuakikisha kuwa wanamuenzi msanii mwenzao
Katika ujumbe aliouandika Swebe, umediriki kusema kuwa soko la filamu bongo limekufa, na kushangaa viingilio vinavyowekwa kwenye kumbi kuhusu kumbukumbu yake ambapo watu hujipatia fedha.