Tanzania Sumatra, imeanzisha msako wa ukaguzi wa leseni za malipo ya mapato kwa ajiri ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya taifa.
Akiongea na mwana repoter wetu Omary Selemani. Mmoja wa maaskali wanao fuatilia utekelezaji wa zoezi hilo la kukamata boda boda, amesema " tumeamua kufanya hivi kutokana na kwamba wamiliki wa vyombo hivyo kukwepa kulipa kodi zao kwa wakati muhafaka".
Lakini kwa upande wa madereva wanao endesha vyombo hivyo maarufu kama boda boda nawao walikuwa na yao ya kusema.
Njame Nasoro ni mmoja wa waendeshaji pikipiki au kwajina lao maarufu kama boda boda, alikuwa na haya ya kusema.
Sisi hatuna tabu kabisa kulipa izo kodi kwani sio bei kubwa sana kivile. Jumla ya deni ambalo mwenye pikipiki analotakiwa kulipa kama kodi ya mapato ni shilingi 23, 000/= tu basi. Kwa upande wangu mimi naona jambo hili sio baya maana ulipaji kodi ni wajibu wetu sote na inaongeza mapato kwa chi yetu.
Lakini ukiachilia mbali na swala hili, sisi waendesha boda boda maisha yetu yanazidi kuwa hatarini zaidi kutokana na kuzuia pikipiki kuingia katikati ya jiji.
Jambo ambalo linazidi kutuweka katika wakati mgumu kimaisha, Kwaiyo tunaiomba serikali ituangalie japo kwa namna moja au nyingine ile ili nasi tuwe na kazi yakuweza kuendesha maisha yetu ya kila siku, kuliko kutuzuia kuendesha pikipiki katikati ya jiji na matokeo yake kuongeza wimbi la majambazi mitaani.