Masahibu yanayowafika watu Sudan Kusini. Watu wa nchi hiyo wamo katika hatari kubwa ya kufa njaa kutokana na mapigano.
kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan Kusini inaelekea kwenye maafa makubwa ya njaa. Mjumbe wa shirika la Misaada ya Chakula Duniani "Welthungehilfe" Jürgen Gihr amesema kwamba bomu la njaa linadunda katika Sudan Kusini na linakaribia kulipuka.
Mjumbe huyo ameeleza kuwa ,kwa kawaida katika nyakati kama hizi wakulima wa nchi hiyo wangelikuwa wanapanda mbegu za mahindi,maharagwe, na mboga mboga kama nyanya na bamia. Lakini mnamo mwaka huu hali siyo ya kawaida hata kidogo. Ameeleza kuwa sasa ni miezi minne tokea majeshi ya serikali yaanze kupambana na wapigajani wa waasi.
Hatua za haraka zinahitajika kuwaokoa watu
Pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka. Ban Ki-moon amesema kwamba, ikiwa hatua hizo hazitachukuliwa mara moja, watu hadi milioni moja watakufa njaa mnamo miezi michache ijayo katika Sudan Kusini.