Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

SAFARI YA MWISHO YA MZEE NGURUMO.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal ndiye aliye ongoza msafara wa mazishi ya mwanamuziki nguli Muhidin Maalim Gurumo yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Masaki Wilaya ya Kisarawe Pwani.

Dk. Bilal aliambatana na viongozi wengine wa Serikali na wasanii mbalimbali katika mazishi ya nguli huyo aliyefariki Aprili 14 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo uliomsumbua kwa muda mrefu.

Akizungumza na mwandishi wetu juzi nyumbani kwa marehemu Mabibo External, msemaji wa familia Yahya Mikole alisema marehemu alitarajiwa kuzikwa jana mchana, nyumbani kwao Masaki kabla ya kusomewa dua asubuhi ya saa tatu nyumbani kwake jijini.

Mke wa mwanamuziki huyo Pili Kitwana akizungumza kwa uchungu, alisema kuwa haamini kama mtu aliyeishi naye kwa miaka zaidi ya 40, amemtoka.“Ninachoweza kusema ni kumshukuru Mungu kwa kuwa kazi yake haina makosa, namuombea apumzike kwa amani.

”Wakati huohuo; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi kwa familia ya mwanamuziki huyo.

“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Muhidini Maalim Gurumo ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wa muziki wa dansi nchini, waliolitumikia Taifa hili kwa bidii tangu miaka ya sitini kupitia sanaa ya muziki katika bendi mbalimbali za muziki wa dansi, kuanzia Bendi ya NUTA Jazz, Mlimani Park Orchestra, Orchestra Safari Sound (OSS) na Msondo Ngoma ambayo ameitumikia hadi alipostaafu mwaka 2013”, alisema Rais Kikwete katika salamu zake.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top