Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

NJIA ZA VIJANA KUFANIKIWA KIMAISHA.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Ukiangalia tabia ya maisha ya mwanadamu utagundua kuwa anafahamu mambo mengi sana, lakini hatendi sawa na ufahamu wake.

Naamini hata vijana wanajua njia za kufanikiwa, lakini hawazifuati.

Kwangu mimi kuwafundisha watu kile wanachokifahamu ni sawa na ujinga. Kamwe siwezi kutumia muda wangu kuwaambia vijana ili waendelee wanahitaji kufanya biashara, kuajiriwa, kujiajiri kulima, kwani kufanya hivyo ni kukosa shabaha ya elimu.

Ukitaka kuthibitisha hili zungumza na vijana wanaoishi maisha magumu uone kama hawatakuorodheshea njia zaidi ya 100 za kufanikiwa kimaisha! Kumbe tatizo lao si kujua bali ni kutenda ambako ndiyo njia ya kuelekea kwenye mafanikio.

Wewe kama kijana jaribu kukumbuka ni biashara, mradi, kazi gani uliyokwishaiwaza na mpaka leo hujaanza kuifanya kwa sababu ambazo hazifahamiki? Miongoni mwa watu wenye tatizo hili wapo ambao si tu kwamba wana wazo, wana pesa, nguvu bali wana uwezo wa kufanya mambo yakawezekana, lakini wamejikuta hawafanyi yale wanayoyawaza na hivyo kubaki watumwa wa umaskini wakiamini tu kuwa, ipo siku wataanza na kufanikiwa.

Tatizo kubwa katika mgando huu wa mawazo ni woga wa kushindwa na ugumu wa kuanzisha jambo. Wanasema waswahili ‘MWANZO MGUMU’ hata hivyo haiwi sababu ya wengi kushindwa kufanya mambo kwa kuhofia kukutana na ugumu. 

Watu wengi waliofanikiwa duniani ni wale ambao walikuwa tayari kuingia katika hatua hii muhimu ya kutenda yale waliyoyawaza na kuyathibitisha kuwa yatasukuma mbele maisha yao.

Wote tunajua mwanzo wa kila kitu ni wazo, lakini mawazo yasiyokuwa na matendo ni sawa na bure! Vitu ambavyo vimekuwepo duniani na vitakavyokuwepo baadaye vitatokana na ushirikiano wa hatua hizi mbili yaani KUAMINI NA KUTENDA.

Ni wakati wako wa kuamini au kugeuza mawazo yako kuwa vitu halisi.Umewaza sana kujenga nyumba mbona hujaanza kujenga? Unasubiri nini kuanza biashara uliyoifanyia utafiti na ukagundua kuwa itakuingizia kipato.

Nani kakuzuia usipange chumba chako na kuanza maisha yako? Amka na uanze kufanya yote uliyoyawaza! unachokichagua Katika hali ya kawaida ndicho kinakuwa, mwanadamu wa kawaida ana mahitaji mengi yanayotoka kwenye vitu vingi pia.

Ukihitaji mchumba kwa mfano, itakulazimu hitaji lako likutane na wingi wa wachumba tofauti tofauti. Changamoto utakayokutana nayo wakati utakapokuwa unataka kutenda ulichoamini ni kuchagua.

Tambua kuwa chochote utakachotaka duniani hakiko peke yake, ukienda sokoni kununua nyanya, utakutana na mafungu mengi ya bidhaa hiyo kiasi cha kukufanya utumie akili kuchagua fungu moja au mawili unayohitaji. Kuwepo na vitu vingi vya kuchangua kama nilivyosema ni moja kati ya tatizo kubwa linalowafanya vijana wengi washindwe kufanikiwa kimaisha kutokana na kutokuwa makini wakati wa kuchagua.

Wapo ambao wameshindwa kuendelea kwa sababu tu walichagua wake wabaya, biashara, fani, kazi, kilimo kibaya na mambo mengine.Inawezekana kabisa pengine hata mambo ambayo yanakuendea kombo leo yametokana na kosa lako la kuchagua.

Ushauri wangu ni kwamba kila mtu anayetaka kufanikiwa kimaisha lazima ahakikishe mambo anayoyachagua yawe ni yale aliyo yahakiki kuwa yanafaa.
Tunachokipata Katika hali ya kawaida hakuna mtu anayetafuta kila siku asipate, hili halina ubishi, labda kinachoweza kuwa tofauti ni kiwango cha kupata.

Sina shaka kuna watu wametafuta sana elimu, kazi, biashara, wachumba, watoto, uongozi na mambo mengine mengi waliyoyahitaji katika maisha yao na kwa kiwango chao wamepata. Lakini tathmini inaonesha kuwa, asilimia 87 ya watu waliopata walivyokuwa wanatafuta hawanufaiki navyo au kwa lugha nyingine kupata kwao hakukuwasaidia.

Mamia kwa mamia ya vijana wametumia au wanatumia mpaka sasa karibu nusu ya maisha yao kutafuta elimu, lakini wanapoipata haiwasaidii wao kama watafutaji, haiwanufaishi wazazi na walezi na haina tija pia hata kwa taifa lao.

Huo ni mfano mmoja, lakini wapo watu wanaotumia muda mwingi kutafuta wasichana wazuri wa kuoa, wanatumia muda mwingi kutafuta pesa, wanajituma kupita katika maofisi na vyeti vyao asubuhi na jioni kutafuta kazi, wakiamini kuwa wakipata wanavyotafuta watanufaika.

Lakini kupata kunapotokea ni wachache wanaoonesha mabadiliko waliyotarajia wao wenyewe au jamii walizotoka na wanazoishi! Ni mara ngapi tumeshuhudia wasomi wakifanya mambo ya ovyo pamoja na elimu zao? Au hatuwaoni watu wanachezea ajira kwa kutojali sheria za kazi, kuwa wazembe, wezi na hata mafisadi?
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top