Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MPIGA GITAA CHIRI CHALLA AFARIKI DUNIA.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mpiga Gitaa wa Skylight Band maarufu kwa jina la Chiri Challa amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia April 17 katika Hospitali ya Muhimbili.

Taarifa za awali zimethibitishwa na uogonzi wa bendi hiyo kuwa mpiga gitaa huyo machachari amefariki baada ya kuugua kwa siku mbili ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake na kuepelekea kutofanya kazi ipasavyo.

Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo Aneth Kushaba AK47 Ugonjwa wa kupooza ulipelekea mishipa ya damu kichwani kupasuka hivyo na kumsababishia maumivu makali sehemu kichwani.

Kutokana na msiba huo uongozi unapenda kutoa taarifa kuwa Show ya Escape One iliyokuwa ifanyike Alhamis ya April 17 imeahirishwa hata hivyo uongozi unasikitika kumpoteza msanii huyo ambaye alikuwa ni kiungo muhimu wa bendi na inaungana na familia ya marehemu Chiri Challa kuomboleza kifo cha mpendwa wao na inatoa pole kwa familia na mashabiki wa Skylight Band na wapo bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.

Msiba na shughuli za mazishi zinafanyika maeneo ya Mwanyamala Ujiji mtaa wa Mpunga. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top