Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili raia wa Kenya Nelson Onyango (43), mkazi wa Kariakoo, jijini Dar es Salaam, dhidi ya mashitaka saba ya udanganyifu.
kutumia kadi zisizosajiliwa, kuingiza nchini na kutumia mitambo ya simu bila kibali, kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuisabishia serikali na mamlaka hiyo hasara ya Sh.
Milioni 6.8 umedai kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Hata hivyo, pamoja na mashtaka yanayomkabili mshtakiwa kuwa na dhamana kisheria mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti ya mahakama anaendelea kusota rumande hadi Mei 3, mwaka huu kesi hiyo itakapotajkwa tena.
Kesi hiyo iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi Devota Kisoka, aliyepangiwa kusikiliza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam hadi Mei 3, mwaka huu.