Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

KABLA YA MELI KUZAMA WANAFUNZI WALITUMA UJUMBE.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Meli ya Korea Kusini iliyokua imebeba zaidi ya abiria 460 wengi wakiwa ni Wanafunzi, ilizama kusini mwa pwani ya nchi hiyo siku ya Jumatano asubuhi ambapo mpaka sasa wengi hawajapatikana huko Korea Kusini ilikozama na ni siku moja tu baada ya ajali ripoti zimeanza kutoka za msg zilizotumwa na wale waliokuwa wamekwama ndani ya meli hiyo.            
                       
Msg ya mwanafunzi mmoja kwa mamaake wakati meli ikizama.Mwanafunzi: ’huenda hii ndio mara yangu ya mwisho kukuambia kuwa nakupenda,’ndio ulikuwa ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa jina Shin Young-Jin kwa mamake. Mama: ”na mimi nakupenda mwanangu,” alijibu mama yake Shin kwa ujumbe wa simu bila kujua kilichokuwa kinaendelea.

Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama huo bado hawajaweza kuwaona watoto wao.

Mawasiliano mengine kati ya mwanafunzi mmoja na babake , yalinukuliwa na shirika la habari la AFP ni haya hapa chiniMwanafunzi: “baba usijali,nimevaa boya la kujiokoa na niko na wasichana wenzangu.

Tuko ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.”Baba: Najua msaada uko njiani,lakini kwa nini hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani ya meli kama unaweza.

”Mwanafunzi: ”Kuna msongamano mkubwa na meli tayari imeanza kuzama”Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado hajapatikana.Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu wapendwa wao.

Katika ujumbe mwingine wa simu, mwanafuzni mmoja alimtumia ujumbe kakake mkubwa meli ilipoanza kuzama.Mwanafunzi: “meli imekwama na haisongi walinzi wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu imetokana na nini’Kakake:” usiwe na wasiwasi fanya kila mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa shwari.

’ baada ya hapo hakukua na mawasiliano mengine yaliyoendelea.Stori imeandikwa na BBC.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top