Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Gor Mahia atangaza hatari.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Kocha Gor Mahia, Bobby Williamson, amewatazama washambuliaji wake, Rama Salim na Dan Sserunkuma, kisha akatoa tabasamu kali na kusema:
“Aisee hawa jamaa hatari, wana kipaji kisicho cha kawaida, wapinzani wakae chonjo.

”Kocha huyo mkongwe alisema kombainesheni ya wachezaji hao pamoja na Shaban Kenga, Patrick Oboya na Innocent Mutiso, inampa matumaini kwamba timu yake itafanikiwa kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Kenya.

Akizungumza baada ya timu yake kuandikisha ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Ulinzi Stars wikiendi iliyopita, kocha huyo alisema siyo siri uwezo binafsi walionao wachezaji hao utaipeleka timu hiyo katika hatua ya hali ya juu.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda, alibainisha kwamba presha itakuwa miongoni mwa wachezaji hao kupata nafasi wakati wanapokutana na timu nyinginezo.

“Tulianza vibaya msimu huu, lakini nina furaha kusema tumeyatatua yale makosa yalikuwa yanatusumbua. Ninawahakikishia mashabiki wa Gor Mahia kutarajia kupata ushindi mfululizo katika mechi zijazo,” alisisitiza.

Aidha Williamson aliutaka uongozi wa klabu kukaza buti kumsaka mdhamini mwingine tangu walipoachwa mayatima na Tuzo ikiwa ni miezi miwili sasa, ili kuhakikisha kwamba hawatatiziki kifedha na hivyo kuathiri viwango vya mchezo wao.

“Aidha ningeomba uongozi wa Gor Mahia kutatua suala la kupata wadhamini ili wachezaji waendelee kupata mishahara na marupurupu yao kwa wakati na bila matatizo,” alisema.

Naye kocha wa Ulinzi Stars, Robert Matano, alisema ilikuwa ni bahati mbaya kwa timu yake kushindwa mbele ya Gor Mahia, lakini anaamini timu yake ni nzuri.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top