Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Azam yasajiri mchezaji kutoka nchini Mali.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Vinara wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wameanza kujipanga tayari kwa msimu ujao baada ya kumsainisha mshambuliaji kutoka Mali, Ismailla Diarra mkataba wa miaka miwili.

Uamuzi huo umekuja kutokana na majaribio ya wiki mbili aliyoyafanya Diarra katika timu hiyo akisimamiwa na kocha wa timu hiyo Joseph Omog raia wa Cameroon.

Taarifa ambazo Mwananchi imezipata kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo umesema Diara aliyekuwa akiitumikia timu ya Bamako de Olyimpic inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo tayari ameshasainishwa mkataba wa miaka miwili kuitumikia Azam.

Kusajiliwa kwa Diarra kunaifanya Azam kukamilisha idadi ya nyota watano wa kimataifa wanaohitajika na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambapo sasa watakuwa na Kipre Tchetche, Kipre Balou na Brian Umony ambaye inaelezwa anaweza kuachwa kumpisha Mganda mwenzake Owen Kasule.

Akithibitisha hilo Katibu Mkuu wa Azam FC, Nasoro Idrissa alisema tayari Azam imeshamalizana na mshambuliaji huyo na wana uhakika wa kuwa naye katika msimu ujao baada ya uwezo wake kumvutia Omog.

“Ninachoweza kusema ni kwamba Diarra sasa ni mchezaji wetu na tutakuwa naye katika kikosi chetu katika msimu ujao wa ligi na mashindano mengine tutakayoshiriki.

Amefanya majaribio na uwezo wake umekubaliwa na kocha wetu Omog,” alisema Idrissa. Wakati huo huo, Doris Maliyaga anaripoti kuwa Azam FC ilitua jana jijini Mbeya kwa jeuri ikiwa na lengo la kuandika historia mbili kwenye Uwanja wa Sokoine ya kwanza ikiwa ni kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara, pili kuwafunga Mbeya City ambao hawajawahi kupoteza mechi hata moja nyumbani kwao.

Matajiri hao wa lambalamba, waliwasili jana jioni na ndege ya Shirika la Fastjet na watacheza na Mbeya City leo, mechi inayotarajiwa kuwa ngumu na ushindani mkubwa kwani endapo Azam watashinda watatimiza ndoto yao waliyoifukuzia kwa misimu miwili walipokuwa wanamaliza nafasi ya pili.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top