Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC, wameingiza nyota wake saba katika kikosi cha timu ya Taifa Stars kitakachoivaa Burundi Aprili 26.
Katika kikosi hicho, ambacho kitaivaa timu ya taifa ya Burundi ‘Intamba Mu Rugamba’ Aprili 26, chini ya kocha msaidizi, Salum Mayanga, amewatema kipa Ivo Mapunda na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Mayanga amewaita makipa wote wa Azam FC, Aishi Manula na Mwadini Ally pamoja na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, wakati mabeki aliowachukua ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba), huku washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Simwanda (Temeke) na Joram Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Kindamba (Temeke), Edward Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Magona (Shinyanga), Omari Nyenje (Mtwara) na Chunga Zito (Manyara).
Washambuliaji ni Mohammed Seif (Kusini Pemba), Ayoub Lipati (Ilala), Abdulrahman Othman (Mjini Magharibi), Paul Bundara (Ilala).
Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo (Tanga) na Bayaga Fabian (Mbeya).Mayanga alisema kuwa kikosi hicho kimeingia kambini kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach.
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
