Ndugu msomaji, usijenge urafiki na starehe wakati shida ni jirani yako, hakuna tuzo za mfanya ngono zaidi ya ukimwi, kaswende, gonorea, kisonono.
Jipange mtu wangu maisha magumu na umri ndo kwanza unazidi kwenda na haurudi nyuma tena.
wazuri ni wengi lakini yupo umpendae zaidi ya wote onyesha kumjali, kumheshimu, kumthamini na kumuonyesha yeye ni wa pekee kwa kumwonyesha upendo zaidi.
Michepuko noma baki njia kuu, ukimuona mwenzi wako hajatulia, mkanye kisha mshauri kiundani zaidi juu ya athali ambazo zitampata baada ya kuanza michepuko.
Ukiona haelekei mwache kisha nenda kapime afya yako ili kujiaminisha zaidi, na subili kwani utampata mwingine atakaekupenda, kukujali na kukuheshmu.
Ndugu msomaji wangu, ungana nami kukomesha mtandao wa ngono, kwani bila ya kufanya ivi hatutakuwa na taifa lililo bora na matokeo yake tutabakia kuwa na taifa duni siku zote.
Kama umeguswa na ujumbe huu Share na mwenzio ili naye aweze kufahamu zaidi, unaweza share ujumbe huu kwenye Facebook, Twitter, Google+, LinkedIn, nakwingineko upendako wewe.