Kundi la mashabiki Manchester United linajiandaa kuchangisha fedha za kutosha kwa ajili ya kukodi ndege ambayo itapita juu ya paa la uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa jumamosi ijayo dhidi ya Aston Villa, ikiwa na ujumbe wa kumsema kocha wao David Moyes.
Mashabiki hao ambao juzi kwenye mechi dhidi ya Manchester City walikuwa wakimtukana Moyes pamoja na kocha wa zamani wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson na hata kufikia hatua ya kutaka kulishusha bango la kumsifu Moyes liliopo kwenye jukwaa la Stretford End.
wanasema wanataka kuonyesha namna walivyochoshwa na kocha huyo.Kwa mujibu wa mtandao wa jarida la mashabiki wa United fanzine, itawagharimu kiasi cha £840 ili kuweza kufanikisha mpango huo siku ya jumamosi na tayari michango ya fedha imeshaanza kukusanywa.