Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

NI AIBU KUONA VINYESI MAENEO YA POSTA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Ndugu mdau karibu sana kwenye ukurasa mpya kabisa unaoitwa Kero Yangu. Ukurasa  huu utakuwa ukichapishwa kupitia Mutalemwa Blog pamoja na Tazama line.

Lengo la ukurasa  huu nikutazama pale palipo sahaulika na kuwakumbusha wahusika ili wakapafanyie kazi. Pia ukurasa huu hauishii hapa Dar es salaam tu, bali mpaka mikoani.

kwaiyo kama kuna jambo ambalo halijawekwa sawa na wahusika iwe ni Serikali,  watu binafsi au taasisi mbalimbali waweza kuwasilisha kero yako na sisi tutaichapisha mtandaoni ili iweze kupatiwa ufumbuzi wakudumu kutoka kwa mlengwa/walengwa/muhusika/wahusika.

Na kwakuanza leo tunajikita katikati ya jiji la Dar hapa maeneo ya Posta mpya. 

Leo nikiwa katika pitapita zangu kwenye mitaa ya posta mpya jijini Dar es salaam,  nimejisikia vibaya sana huku nikiwa nimegubikwa na aibu kubwa baada ya kukutana na station chemba

katikati ya barabara ya Kisutu ikiwa inatoa maji yenye vinyesi na kusambaza maji hayo mtaani, huku harufu mbaya ikitanda eneo lote linalozungukwa na maji hayo machafu.

Huku barabara ikiwa inatumiwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi mbalimbali wa nchi hii, wakati barabara izi zikiwa na mashimo makubwa.
Kiukweli inasikitisha sana maeneo ya posta kuwa katika hali kama hii, ambapo ndipo panatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa sababu maghorofa makubwa na sehemu ambapo panapatikana bidhaa original ndio huku bila kusahau maofisi ya watu maarufu nk.

Nawaomba wahusika kwenye eneo zima la posta mpya jijini Dar es salaam muweze kurekebisha maeneo yote yenye kudhalilisha na kuaribu sifa ya eneo hili maarufu jamani.
Pia ikumbukwe kuwamba sio maeneo haya pekee bali yakomengine mengi zaidi ila kwa leo naishia hapa. Endelea kutembelea Mutalemwa Blog kwa habari zenye tija kwa jamii yetu.

Kwa maoni/ushauri au kero yako basi waweza kutuma ujumbe wako kwa sms au what's up  kupitia 0659919292 kumbuka kutaja majina yako kamili na sehemu ulipo kisha ujumbe wako tutauchapisha na utawafikia wahusika. 
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top