Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MHE. MAGUFULI AKIMBIWA NA VIGOGO WA WIZARA YAKE LEO

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Baadhi ya vigogo katika Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli (pichani), wameikimbia wizara hiyo na kwenda sehemu nyingine kwa kile walichodai ni uongozi wa kibabe na unyanyasaji katika idara ya usalama barabarani na mazingira.

Uchunguzi unaonesha kuwa wizarani hapo umebaini kuwa katika idara hiyo inayoongozwa na Julius Chambo kama Kaimu Mkurugenzi imekimbiwa na vigogo watatu, Juma Kijavara, Omari Kinyange na Samson Nkundineza ambao wameondoka wizarani hapo ndani ya mwezi mmoja, Desemba mwaka jana 2014.

MHE. MAGUFULI AKIMBIWA NA VIGOGO WA WIZARA YAKE!

 Waziri ya Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli.

Vyanzo vyetu vya habari ndani ya wizara hiyo vinadai kwamba tangu Chambo ahamishiwe katika idara hiyo akitokea kituo cha mizani Himo mkoani Kilimanjaro, utendaji wa kazi umekuwa ukisuasua kwa kile kinachodaiwa kuwa ni uongozi wa kidikteta pia wameona kama amewekwa hapo kiupendeleo kwa vile mambo ya utawala hajui.

Katika idara hiyo inayoongozwa na Chambo ilikuwa na wahandisi wanne lakini baada ya kuondoka kwa hao watatu alibakia mmoja na inasemekana wameletwa wengine kufidia walioondoka. Kuhama kwa vigogo hao kumewatia hofu wafanyakazi waliobaki na inasemekana kuwa baadhi yao wanataka kuondoka.
Aidha baadhi ya wafanyakazi wamelalamikia kipindi kirefu alichopewa kukaimu nafasi hiyo.

“Huwezi kukaimu ofisi kwa muda mrefu namna hiyo  hapa kuna tatizo,” alisema mhandisi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina lake mtandaoni. Aliongeza kuwa kama wizara haitafanya mabadiliko stahiki kuna wahandisi watatu wataondoka hivyo wizara kupoteza wataalamu wazoefu kitu ambacho kitaleta shida kubwa wizarani hapo.

paparazi alipomtafuta Chambo ofisini kwake alikiri kuondoka kwa vigogo hao na akadai kuwa ni mmoja tu ndiye aliyemuaga lakini wengine hawakufanya hivyo.
“Mimi naamini wameondoka kwenda kutafuta maslahi zaidi, kuhusu madai mengine mimi siwezi kuzungumzia masuala ya wizara, nendeni kwa katibu mkuu,” alisema Chambo. Naye katibu mkuu wa wizara hiyo, Musa Lyombe alipohojiwa alisema wafanyakazi hao wameondoka Desemba mwaka jana lakini hata yeye ameshangazwa na kuondoka kwao.

“Nafikiri kuna jambo na kuna umuhimu wa kulichunguza suala hili kwa karibu, wao walikuja kwangu nikijua wanafuata maslahi, kwa nini itokee katika idara hiyo moja?” alihoji.



Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    
In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top