Utekelezaji wa shinikizo la kuvuliwa madaraka kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo linaloendelea kutolewa na Wabunge na kwa baadhi ya wanasiasa kwa Rais Jakaya Kikwete huenda ukaacha msononeko kwa wananchi walionufaika kwa kipindi kifupicha uongozi wa Waziri huyo.
Muhongo aliyejitengenezea uadui na wafanyabiashara na wanasiasa kutokana na misimamo yake ya kulinda maslahi ya umma na kuzungumzia ukweli huku akijiamini kulikotafsiriwa kuwa ni dharau hatma ya uongozi wake po mikononi mwa Rais ambaye ameshauriwa na Bunge kutengua uteuzi wake.
Baadhiya wananchi walisema Waziri huyo amefanya kazi kubwa na ya kimaendeleo kwa kipindi kifupi alichopewa majukumu na moja ikiwa ni kusambaza umeme katika vijiji vingi na kudhibiti ubadhirifu uliokuwepo hapo awali.
Piaamefanya juhudi kushawishi Watanzania ambao ni wataalam wa gesizaidi ya 10 wanaofanya kazi nje ya nchi hususani Canada na Uingereza mpaka wakakubali kurejea na kufanya kazi hizo nchini.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgqkfvdsCQnPtVtdB1BRo8WNnIXPkLftFAgnwnEsIn6wi5e6a3eWRGwII7wh1RRZiR7YnhR6IfHZu2S-L5TKd4i4JeqIXAZnEeqqNhmqdzjNYA4Q76BTKpB9MmvWIsr0dnAZXNg5DJSgT0/s200/FLASH+NECTA.gif)
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.