Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MWANAJESHI ALEWA POMBE NA KULALA KTK MAJI MACHAFU

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
kATIKA hali isiyotegemewa askari mmoja wa jeshi la kujenga Taifa (JKT) anayesadikika kuwa na wa kambi ya Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa usiku wa leo amenusurika kuvuliwa nguo za jeshi hadharani baada ya kukutwa amelewa chakali na kulala katika mfereji wa maji machafu eneo la nje ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa.



Tukio hilo lilitokea muda wa saa 2 usiku baada ya wasamaria wema kumshusha askari huyo kutoka katika basi la Mgumba ambalo alikuwa amepanda kutoka Mafinga kuja mjini Iringa.

Akisimulia kisa na mkasa wa askari huyo kulewa chakali kiasi cha kushindwa kujitambua mmoja kati ya wasamaria wema aliyejitolea kumshusha katika basi hilo alisema kuwa askari huyo alipanda basi hilo Mafinga huku akiwa amelewa na wakati wote wa safari alionekana akinywa pombe kali kiasi cha kushindwa kujimudu na kuanza kutapika na kujisaidia haja ndogondani ya basi hilo.


Hata hivyo alisema baada ya kufika stendi ilikuwa ni vigumu kujitambua hivyo kupoteza fahamu na kulazimika kumpa msaada na kumzimua kwa maji kabla ya kupata fahamu kiasi na kujificha chini ya mfereji wa maji machafu.



Alisema kuwa mara baada ya kujitambua kiasi aliweza kutoa namba ya ndugu yake ambae ni askari wa FFU mjini Iringa aliyefika kumnusuru kuvuliwa nguo na kiongozi wake aliyefika eneo hilo na kumkutana akilishushia heshima jeshi kwa ulevi uliopitiliza.


"Umelidhalilisha sana jeshi kwa askari kulewa hivi ukiwa katika sare, sasa nataka kukuvua sare kisha nakupeleka kulala polisi kabla ya kesho kukuchukulia hatua zaidi " alisikika akisema kiongozi huyo ambae jina wala cheo chake hakukitaja.

Maamuzi hayo ya kiongozi wake yaliwafanya mashuhuda kumuangukia na kumwomba amsamehe kwani bado ni kijana mdogo sana maombi ambayo aliyakubali na ndugu zake kumpakiza katika Taxi na kumpeleka eneo la Kihesa.

Ushauri wetu kwa askari wetu kujaribu kuheshimu nafasi hizo japo hakuna anayewakataza kunywa pombe ila watambue kuwa unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ama chonde chonde ulevi noma. 
 


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    
In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top