![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSyoCZw4WbMQc0604udwmgtk1i7QGUF8Ml1yO5GqUlLhO_pz0mf-oPefoQLNnGCSLfvLe1QvbUhNTSUKEcjpzbYw3RFvBCjiQyYUicwDLi9q6oqrFE-XERJvuahHB8rD6ixUGTt6DwDcc/s1600/mimi.jpg)
Kennedy Elimeleck Ndosi ambaye ndiye mmiliki wa blogu maarufu ya www.masamablog.comunayosomwa na watu zaidi ya 30,000 kwa siku akiwa na tuzo yake aliyotunukiwa kama Kiongozi bora baada ya kuibuka mshindi kati ya wanafunzi 68 wa Diplomasia waliopigiwa kura na yeye kuibuka Mshindi wa tuzo ya kiongozi bora yaani Best Leadership Diplomatic Award 2013/2014 iliyotolewa na Chuo cha kimataifa cha Diplomasia Jana jijini Dar es Salaa ambapo ilidhaminiwa na Ubalozi wa Irani,Umoja wa Ulaya(EU),UN,Coca Cola,Forever Living Products Tanzania Ltd,Ubalozi wa Marekani na mashirika mengine ya Kimataifa.
Kennedy Elimeleck Ndosi akiwa na Diwani wa kata ya kipawa jijini Dar es Salaam Mhe.Bonnah Kaluwa ambapo naye alishinda tuzo ya mwanfunzi aliyetoa mchango mkubwa kwa wanafunzi wenzake katka chuo hicho ambapo amemealiza kozi ya Post graduate in management of Foreign Relations.
Kennedy Elimeleck Ndosi akiwa na rafiki yake aliyeshinda tuzo ya kiongozi mwenye maadili Bw.Ismail Shah ambaye
pia
aliwahi kuwa Rais wa serikali ya wanafunzi.
Kennedy Elimeleck Ndosi na Kaimu Mkuu wa chuo cha Diplomasia Dk Benard Archiula na Rais wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho (George Faustine)..Alisema..''Namshukuru Sana Mungu kwa Wema wake...Nashukuru sana Uongozi wa chuo Cha kimataifa cha Diplomasia(CFR) kwa kutambua mchango wangu katika Uongozi wa serikali ya wanafunzi..leo nimepewa tuzo ya Uongozi bora wa uwakilishi kidiplomasia Yaani Best Diplomatic Leadership Award 2013/2014..Asanteni sana wenzangu kwa kunipa tuzo hii kwani nnamini Kila kitu hupangwa Na mungu....Namini Iko siku nitapewa tuzo kubwa zaidi ya hii kitaifa na kimataifa..asanteni sana
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgqkfvdsCQnPtVtdB1BRo8WNnIXPkLftFAgnwnEsIn6wi5e6a3eWRGwII7wh1RRZiR7YnhR6IfHZu2S-L5TKd4i4JeqIXAZnEeqqNhmqdzjNYA4Q76BTKpB9MmvWIsr0dnAZXNg5DJSgT0/s200/FLASH+NECTA.gif)
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.