Watu wengi wamekuwa watumiaji wa usafiri wa anga Tanzania kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na miaka ya nyuma ilivyokuwa, lakini good news ya leo imeripotiwa na kituo cha ITV ambapo idadi ya mashirika ya ndege kutoka nchi mbalimbali imeongezeka na kufikia 18.
Hii ni moja ya habari nzuri kwa wale wote ambao wanatumia usafiri wa anga kwa Tanzania ndani ya mwaka 2014.
Kuongezeka kwa mashirika hayo kunafanya kukua kwa huduma hiyo na kurahisisha huduma hiyo kwa wasafiri, lakini hata Serikali pia inapata pato linalotokana na malipo ambayo kila ndege inayotua inalipia tozo ambapo malipo hayo huzingatia uzito wa Ndege.
“… Tunafanya kazi na mashirika haya tunazungumza nao, tumeajiri Consultant ambaye ndio kazi zake hizi routs, tumekaa naye yeye ndio anazionyesha hizi Airline kwamba ukienda Dar es Salaam utapata abiria hawa na hawa… siyo inakuwa mtu anakaa tu nyumbani anaota ndege zinakuja… kazi inafanyika chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgqkfvdsCQnPtVtdB1BRo8WNnIXPkLftFAgnwnEsIn6wi5e6a3eWRGwII7wh1RRZiR7YnhR6IfHZu2S-L5TKd4i4JeqIXAZnEeqqNhmqdzjNYA4Q76BTKpB9MmvWIsr0dnAZXNg5DJSgT0/s200/FLASH+NECTA.gif)
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.
In order you follow me just click one of the Icon Button above.