Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

John Mnyika-wananchi mwandikie barua Jk

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amewashauri wananchi wanaoishi kandokando mwa hifadhi ya Barabara ya Morogoro kumwandikia Rais Jakaya Kikwete barua  kuhusu mgogoro uliopo katika barabara hiyo.

Mnyika alitoa ushauri huo katika mkutano uliofanyika Luguruni Park, Dar es Salaam ambao ulihudhuriwa na wawakilishi wa  wananchi  zaidi ya 5,000 wanaoishi  kandokando mwa barabara hiyo ambao nyumba zao zimewekewa alama za ‘X’ na Wakala wa Barabara (Tanroads)  kwa ajili ya ubomoaji.

Alisema haoni haja ya kupanua barabara kutoka Kibaha hadi Dar es Salaam wakati maeneo mengine ya nchi hayana barabara zinazopitika kwa kirahisi.Alisema upanuaji wa barabara hiyo unakiuka amri halali ya mahakama iliyoamuru Tanroads kusitisha zoezi hilo, kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa mwaka jana na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.

Mwenyekiti wa  Kamati  ya waathirika hao, Chrizant Kibogoyo, alisema wamemiliki ardhi hiyo kihalali zaidi ya miaka 30 hadi kufikia mwaka 2000 ambapo Waziri John Magufuli aliagiza Tanroads kuingia katika ardhi na makazi yao hadi mita 120 toka katikati ya Barabara ya Morogoro pande zote mbili kuanzia Kibaha hadi Tamco.

Kibogoyo alisema uingiaji huo si halali, kwani  haukuheshimu hatimiliki zilizotolewa na Wizara ya Ardhi yenye dhamana kwa mujibu wa sheria za nchi kuthibitisha umilika wa ardhi.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top