Joh makini: katika kipindi cha hivi karibuni, muziki wa hip hop hapa nchini umeendelea kufanya vyema sokoni, kutokana na kushika kwa kasi kubwa sana ya wapenzi wa miondoko hii ya hip hop.
Hata ivo kama wasemavyo wahenga, ya kwamba katika msafara wa mamba kenge hawakosi, kutokana na malalamiko na kero mbalimbali zinaelekezwa kwa baadhi yao kukosa ubunifu na kusababisha kuimba nje ya misingi ya hip hop, pamoja na pumba nyinginezo nyingi.
Kauli hii inaungwa mkono na mmoja wa wanamziki wa hip hop wanaofanya vizuri katika soko hilo, akijitambulisha kupitia nyimbo zake mbalimbali ikiwemo ya Hao, chochote, bye bye, sijutii na nyingine kadhaa.
Huyu sio mwingine bali na mzungumzia Joseph Simon, maarufu kama joh makini, mwamba wa kaskazini anayewakilisha kundi la weusi, linaloundwa na wasanii wengine kama Nikki wa pili na Gnako.
Joh makini anaendelea kusema, mziki wa hip hop una changamoto nyingi sana, kwaiyo anaomba washabiki na wasanii wote wa hip hop kwa ujumla waheshimu tasnia hii, maana bila ya kufanya ivyo hakutakuwepo tena hip hop flavour.
