Kuzinduliwa kwa sherehe za Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God zilizofanyika Mkoani Mbeya siku ya Jumamosi wiki iliyopita na kuhudhuliwa na watumishi wa Mungu mbalimbali wakiwepo Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dr Barnabas Mtokambali,Makamu Askofu Mkuu wa TAG Rev Dr Magnus Mhiche,Katibu Mkuu wa TAG, Rev. Ron Swai na kaimu Askofu Mkuu Msaidizi wa kanisa la EAGT Mchungaji.
Mwaisabila sherehe hizo za Miaka 75 ya TAG zinategemewa kufikia kilele chache mwezi wa saba waka huu 2014.Katika Siku hiyo kulitanguliwa kuzinduliwa kwa Jengo jipya la Kanisa la Shillo huko Mbalizi ambalo inaaminiwa kuwa Kanisa la kwanza la TAG mkoani mbeya, Askofu Mkuu wa TAG .Dr Barnabas Mtokambali ndiye aliye zindua jengo hilo na kuweka jiwe la Msingi.
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa MkoaMbeya Abbas Kandoro aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya mbeya vijijini.Pia sherehe hizo ziliudhiliwa na Wamissionary wa TAG kutoka Marekani kuhudhulia tukio hilo.
