Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

NDOTO

KUTEKA MAJI KISIMANI.
kama mtu ataota anateka maji kisimani na maji hayo wakapewa watu kuywa, maana yake ni kuwa atakuwa ni sababu ya kuwalea mayatima, qatu dhaifu, na maskini kupata maisha ya kujikimu. Pia ina maana kuwa ataishi maisha ya uchaMungu huenda mali yake inaweza kuwa ni sababu ya watu kwenda Hijja.
KUMWAGILIA MTI.
Kuteka maji kisimani na kuwapa watu kunywa,  maana yake nikuwa mtu mwenye kufanya hivyo atawasaidia watu kwenda hijja.
TAKA NDANI YA MAJI.
Kuteka maji kisimani na kuona taka au najsi ndani ya hayo maji, tasili yake ni kwamba mtu mwenye kufanya hivyo ataichafua mali yake kwa mali ya haramu.
NDOO ILIYO VUNJIKA.
Kama mtu ataota ndoto kuwa ndoo iliyotumika kutekea maji inaonekana kama kuvunjika, maana yake ni kuwa msaada aliokuwa anatoa kwa watu utakoma.
KUANGUKA NDANI YA KISIMA.
Kushuka ndani ya kisima au kuanguka ndani yake,  maana yake ni kwamba mtu huyo atakumbwa na uzuni pamoja na masikitiko,  lakini mwishowe atapata furaha na raha kutokana na ushindi wake. Hii inatokana na kisa cha Nabii Yusuf.
KUTUMBUKIA MTONI.
Kama mtu ataota ndoto kuwa yeye mwenyewe anatumbukia au anaingia mtoni atakuwa na wasiwasi na hofu maana yake nikuwa hivi karibuni atakumbwa na huzuni pamoja na masikitiko.
KUNYWA MAJI MACHAFU TOKA MTONI.
Endapo mtu ataota anakunywa maji machafu au matope kutoka mtoni yeye mwenyewe, maana yake nikuwa atakabiliwa na huzuni, maumivu na maumivu hayo, kiwango chake cha maumivu na huzuni kitategemea kiwango cha maji aliyokunywa.
KUOGA MTONI.
Kuoga mtoni katika ndoto au baharini bila ya hofu yeyote, wasiwasi au fedheha maana yake ni kukombolewa kutokana na matatizo kama mwotaji wa iyo ndoto alikuwa anaandamwa na huzuni, huzuni wake utaondolewa mahala pale kisha itakaa furaha, kama anaugua maradhi atapona, kama yupo katika mazingira ya taabu MUngu atampa nafuu, ksms anasumbuliwa na madeni Mungu atamwezesha kulipa madeni hayo, kamq yupo kifungoni (gerezani) Mungu atampa uhuru wa kumwezesha kutoka kifungoni.
KUVUKA MTO.
Ukiota ndoto kuwa unavuka mto au mtu yeyote anavuka mto au mkondo wa maji, tafsiri yake ni kwamba wewe au yule uliye mwota ndotoni atapata kuwa na nafuu kutokana na huzuni, masikitiko na hofu. Lakini kama mto huo au mkondo huo wa maji una matope,  uchafu au unaendelea kujaa, maana yake nikuwa mwotaji wa ndoto hiyo atavunja uhusiano wake na jirani yake,  kijana wake wa kiume au rafiki yake wa karibu na kuanzisha uhusiano mpya na mtu mwingine. Badala ya hii atakutana na mtu ambaye uhusiano wake utakuwa wa kukalifisha.
ZIWA AU BAHARI.
Kuota zowa au bahari maana yake ni ufalme mkubwa, utawala wa nguvu, na saba ikiwa kama hauna uchafu, matope au mawimbi ya kutisha kuonekana katika ndoto hiyo.
KUNYWA MAJI YA BAHARI.
Kama mtu ataota anakunywa maji ya baharini,  na mqji hayo hayana matope au uchafu au hakuna maji hayo machafu, maana ya ndoto hiyo nikuwa atapata mali nyingi kadri ya maji aliyokunywa. Pia atakuwa na maisha mazuri na ya furaha. Lakini kana maji hayo aliota yana chumvi chumvi au uchungu au bahari imefunikwa na kiza au maji yanatengeneza mawimbi makubwa yakutisha, tafsiri yake nikuwa atasumbuliwa na huzuni, khofu na taabu, ukubwa wake utategemea kiasi cha hali hizo jinsi zilivyo tendeka ndani ya maji au bahari.
KUZAMA MAJINI.
Kuzama ndani ya maji ya bahari yenye maji masafi humaanisha kuwa mwotaji wa ndoto hiyo ATAZAMA katika mambo ya utawala au serikali. Lakini kama maji ni chumvi chumvi au yana taka, maana yake nikuwa atakabiliwa na taabu ambayo itamsababishia kuangamia.
KUTEMBEA JUU YA BAHARI.
Ukiota unatembea juu ya bahari,  tafsiri yake ni kuwa utawala juu ya watukufu na tabaka la watu wasomi wa kidunia.
CHOMBO CHA USAFIRI WA MAJINI.
Chombo kinachotembea baharini kwa kawaida humaanisha ukombozi na Usalama kutokana na mabalaa. Wakati mwingine hufasirika kama sababu ya kumfikia mfalme au kuwa karibu naye sana au kumtumikia. Wakati mwingine inasemekana pia itatafsiriwa kama huzuni na mashaka ambayo yatafikia mwisho wake.
KUINGIA AU KUKAA KWENYE CHOMBO CHA USAFIRI WA MAJINI.
Kama mtu ataota ndoto hii yeye mwenye kama amepanda ndani ya chombo cha usafiri wa majini ambacho kina kwenda tuu majini, maana yake ni kuwa ataingia matatizoni na mfalme au mamlaka kiasi cha kumpeleleza. Uzito wa upelelezi utategemea ukubwa wa chombo cha usafiri. Mwisho atakombolewa kutokana na kukamatwa.
MAJI NDANI YA CHOMBO CHA USAFIRI WA MAJINI.
Kupanda au kukaa ndani ya chombo cha usafiri wa majini kilicho jaa maji, maana yake ni huzuni,  masikitiko, mashaka,  balaa, kifungo au ugonjwa.  Lakini matokeo ya mwisho itakuwa ni ukombozi wa nusra.
KUSHUKA KUTOKA NDANI YA CHOMBO CHA USAFIRI WA MAJINI.
Kushuka au kuondoka ndani ya chombo cha usafiri wa majini ni ishara ya kunusurika na mambo mabaya au balaa.
CHOMBO CHA USAFIRI WA MAJINI JUU YA ARDHI KAVU.
Kama kuna mtu ataota ndoto ya namna hii kuwa chombo cha usafiri wa majini kinamsogelea, taarifa nzuri kuwa mapema atapata ufumbuzi wa matatizo yake na atanusurika na mashaka.
MKONDO WA MAJI.
Mkondo wa maji au kijimto kidogo ambacho kwa kawaida mtu huwezi Kuzama ndani yake tafsiri yake ni sawa na mto isipokuwa kwamba katika ndoto nyingi humaanisha taarifa njema na maisha mazuri na safi.
MAJI NDANI YA SUFURIA AU BAKULI.
kama mtu ataota ndoto kuwa yeye mwenyewe anabeba au anamiliki maji yaliyo ndani ya sufuria ay bakuli na akawa na yakini kuwa yako twahara au yuko safarini katika sehemu ngeni na isiyofahamika, basi maji hayo ndani ya bakuli humaanisha muda wake wa maisha. Kama ataota anakunywa maji yote basi muda wake wa maisha utakuwa umetimia, sasa anatakiwa ajiandae kwa ajiri ya akhera, kama ata kunywa sehemu ya maji inamaana atakuwa na idadi ya miaka kadhaa ya kuishi. Tafsiri hii pia itatolewa kama badala ya maji, kilichomo ndani ya sufuria au bakuli ni mchuzi.
UDONGO WA MATOPE.
Hii katika ndoto humaanisha huzuni, masikitiko na hofu. Kiwango cha ukubwa wake (huzuni, masikitiko na hofu) hutegemea na jinsi ya ukubwa wa udongo wa matope ulivyo one kana ndotoni.
MAJI YA MOTO.
Maji ya moto katika ndoto humaanisha huzuni iliyo sababishwa na mfalme,  matawala au mamlaka ya Serikali. Kadri maji yatakavyo kuwa moto zaidi ndivyo pia huzuni itakavyo kuwa kubwa. Wakati mwingine,  maji ya moto humaanisha khofu,  fadhaa au ugonjwa.
TOFALI.
Tofari ambalo limechomwa au kukaushwa juani kiasi kwamba sio tena udongo, mara nyingi humaanisha mali ya mtu ambayo alichuma. Kupata sehemu ya tofari humaanisha kuwa mwotaji wa ndoto hiyo atapata mali iliyo chumwa.
TOFALI KUANGUKA TOKA UKUTANI.
Ukiota ndoto ya namna hii jua kwamba mwanaume au mwanamke atatoka katika familia yake atapotea au kukimbia au kufariki dunia kabisa.
BAAFUNI.
bafu au maji ya moto ya kuoga humaanisha huzuni inayo sababishwa na wanawake. Lakini Kwakuwa ni kawaida mtu hutumia mda mdogo bafuni maana yake ni kuwa huzuni wake utakuwa wa mda mfupi.
KWENDA HAJA NDOGO BAFUNI.
kwenda haja ndogo bafuni au kunyoa nywere kwa vifaa vyovyote vya kunyolea ni ndoto nzuri.  Kama mwotaji wa iyo ndoto yupo kwenye mateso, basi mapema atapata nafuu, kama yupo kwenye hofu, mapema atapata furaha, kama mezongwa na huzuni, huzuni wake utaondoka mapema na kama ni ugonjwa atapona mapema na kupata afya nzuri.  Kama hauna hali zozote hizo zilizotajwa maana yake ni, kama si magonjwa,  atakuwa mgonjwa, kama anafuraha basi atazongwa na huzuni, aidha kutokana na hasara za kifedha.
UPEPO WA DHORUBA.
Upepo unao vuma katika hali ya kawaida bila ya alama yeyote ya kiza huwa ni ishara ya baraka juu yako wewe mwotaji.

KIPANDE CHEMBAMBA CHA ARDHI.
Kama ardhi ni ndogo humaanisha mwisho wa maisha, ndoto hiyo hiyo pia inaweza kumaanisha wilaya kama mwotaji wa ndoto hiyo anastahili nafasi hiyo, wilaya inaweza kutafsiriwa kama ofisini palipo na utawala,  matawala,  mamlaka,  sheria na zenye kufanana na hayo.

KUSIMAMA KATIKA ARDHI KUBWA NYOOFU.
Kusimama katika ardhi kubwa nyoofu humaanisha kuwa maisha ya amani ya ajabu yanakusubili wewe mwotaji wa ndoto hiyo.  Pia humaanisha usalama,  ulinzi,  amani pamoja na mapatano.

KUFANYA MAZUNGUMZO NA DUNIA.
Kuota ndoto dunia inamuongelesha mtu humaanisha kuwa atapata ustawi mzuri kiasi kwamba itasababisha watu washangae na kustaajabu. Tafsiri hiyo hiyo pia hutolewa pindi kitu kinaonekana kumwongelesha mtu hali ya kuwa kitu hicho huwa hakizungumzi.

KUDIDIMIA ARDHINI.
Kama mtu ataota ndoto kuwa yeye mwenyewe anatokomea ardhini bila ya kuwepo kaburi, maana yake ni kuwa atajiangamiza mwenyewe kwa sababu ya tamaa ya mambo ya kidunia.

DUNIA KUZUNGUKA.
Kama mtu ataota ndoto kuwa dunia inamsababishia kuzunguka, maana yake ni kwamba mambo yake yatabakia kuwa na vurugu kubwa na mkanganyiko,  jambo ambalo litamsababishia kukimbia kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kutafta maisha.

KUPITA NDANI YA PORI, NYIKA NA JANGWA.
Kama mtu ataota ndoto yeye mwenyewe anapita ndani ya pori, nyika, au jangwa katika namna ambayo haipotei inamaana atabaki na msimamo madhubuti juu ya dini yake. Kama atapotea ina maana ana mashaka na dini yake.

MILIMA NA VIJILIMA.
Milima na vujilima humaanisha watu, vyeo vyao pamoja na nafsi zao kutegemeana na ukubwa. Urefu na wingi wa milima na vijilima hivyo. Tafsiri hiyo pia hutolewa kwa kuota jabali na miamba. Mtu ataota ndoto hiyo atapata heshima na kutukuzwa milele yote.

KUPANDA MLIMA AU MILIMA.
Kama ukilala na ukaota kuwa unapanda mlima au milima,  maana yake ni kuwa utafika katika nafasi zajuu katika utawala.

MIAMBA NA MAWE.
Kuota mawe au miamba,  humaanisha ugumu wa moyo, ukorofi, ukatiri na kiburi.

CHANGARAWE.
Changarawe humaanisha usengenyaji na kutoa shutuma dhidi ya mtu fulani.
KUSIMAMA JUU YA MLIMA KILELENI.

Kama ukilala na ukaota kuwa umesimama juu ya mlima kileleni, humaanisha kuwa utamshinda nguvu mtu mwingine ambaye ana cheo au nafasi kama yako.

KUCHIMBA SHIMO NDANI YA MLIMA.
Kama utaota unapasua na kuingia ndani ya mlima (kama ambavyo mwizi uvunja nyumba na kuingia) inamaana una hatia ya kumpotosha mtu yeyote yule wa karibu.

KUPANDA MLIMA BILA YA KUGUGUMIA.
Endapo utaota unakwea mlima bila ya kugugumia ni ishara kuwa tamaa yako ni kupata kitu itafanikiwa lakini badala ya tabu pamoja na shida nyingi.

KUPANDA JUU.
Endapo ukiota unapanda juu kama ilivyo katika maisha maana yake ni kuwa utapata heshima na kutukuzwa na utaweza kupandishwa cheo. Upandaji huo hutamaniwa sana kwa ujumla,  upandaji au ukweaji humaanisha heshima ya mtu na utukufu duniani na katika mambo ya kidini. Wakati mwingine kupanda mlima au mti humaanisha kuwa mwotaji atajaliwa ulinzi dhidi ya mabalaa ya aina zote.
Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top