Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

TAFADHALINI UKUTA WEKENI KANDO MFANYE MAZUNGUMZO MEZANI.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Yes sikulilia ndani alipoingia matatizoni. Niligangamala nikapaza sauti na wanangu mchana kweupeee. Haikuwa rahisi hata kidogo lakini ilinibidi kujitoa fahamu kwa ajili ya kuokoa familia yangu.


Leo napoona dalili nyingine za kuingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya, kamwe siwezi kukaa kimya. Yes sintakaa kimya nimwache aende kutumbukia shimoni nitamwambia bila aibu kama nilivyompigania bila aibu.

Dear love, umenikasirikia sana kwa kitendo hiki ninachofanya... Lakini naomba ukumbuke wakati unapitia matatizo, ni Mimi nilikuwepo na wewe wakati wote mpz wangu mtoto nililazimika kumwachisha ziwa akiwa mdogo sana akalia sana akazoea nikamwacha na Dada kila ilipokuwa tarehe ya kesi nikaja kukutia moyo mpz wangu Tabora mbali kote.

Nikajikaza sanaaaa, kukuonyesha tabasamu ili kukupa Amani japo njia nzima nililia sana kwa uchungu ulilia kila uliponiona mimi nilijikaza sikulia mbele yako ili nisikuache na mawazooooo.

Kila nilipokuja Gerezani kukuona uliwaulizia rafiki zako ulokuwa unawaamini sana, tena uliamini wangekuja kesho yake, hukuwaona mpaka ukatoka. ulikuwa unawaulizia kama wamenitafuta, nilikujibu hakuna aliyenitafuta mpenzi ukaumia sana mpenzi wangu. Kuna wengine hukutaka hata kuongea nao baada ya kutoka ndani na kurudi uraiani.

My love, Siko tayari kupitia mateso niliyopata love, siko tayari kukuona katika mazingira magumu kama yale mbaya zaidi ni ya KULAZIMISHA. Labda yatokee bahati mbaya. Lakini ya kwenda kuyatafuta hapana baba. Najua tena nauhakika hauko tayari kuniona tena katika mateso kama Yale, hilo nauhakika nalo.

Nimewaambia watoto wanisamehe kama nitakuwa nimekosea, lakini naimani hata wao cha moto walikiona, wasingependa baba yao aingie tena kwenye shida kama ile au zaidi ya ile.

Popote ulipo jua nakupenda sana ndo maana nakulinda mume wangu kwa garama yeyote.

Kwangu Mimi Familia kwanza, Taifa kwanza, chama baadae. MSIFANYE UBABE TULIZENI JAZBA KWA FAIDA YA FAMILIA ZENU NA TAIFA ZIMA KWA UJUMLA WAKE.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top