Wananchi zaidi ya 400 wa vijiji vya Geterere na Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara waliokuwa na hasira wamevamia nyumba mbili za wakazi wa kijiji cha Geterere na kuzibomoa na kisha kuziteketeza kwa moto nyumba hizo pamoja na samani zake wakimpinga mkazi huyo kutii amri ya mahakama inayomtaka kubomoa makazi yake katika eneo la Josho alilokuwa akiishi kwa takribani miaka 10 kuondoka.
ITV ilishughudia zoezi hilo likiongozwa na maandamano ya akinamama waliokuwa wakiimba na kuanza kubomoa nyumba hizo huku familia yenye watoto 10 wakilazimika kukimbia kuepuka kuuwawa na wananchi hao wanaodaiwa si wanakijiji na pia walidaiwa kuvamia eneo hilo baada ya kubomoa miundombinu ya Josho na sasa hawana eneo la kuogeshea mifugo yao.
ITV ilizungumza na Bw Raphael Philip akiwa mbele ya mikono ya polisi waliokuwa wamefika katika eneo hilo baada ya kukuta wananchi hao wameshatekeleza azma yao na kudai kwamba eneo hilo ni mali yake na kuwatupia lawama mwenyekiti wa serikali ya kijiji, Diwani pamoja na polisi kuchelewa kufika eneo la tukio.
Hata hivyo Diwani wa kata ya Geterere Bw Petro Lory amesema wananchi hao hawakuhamasisha bali walilazimika kuchukua uamuzi huo kupitia vikao vya mila, huku mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Fabiano Gurt amedai wakazi hao wawili walivamia na hawakupewa eneo hilo kupitia vikao vya mikutano mikuu ya kijiji.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies