Featured

    Featured Posts

Loading...

MHE. PAUL MAKONDA AWASAINISHA WATUMISHI WOTE WA DAR, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda amewasainisha mkataba wakuu wote wa idara kusimamia na kuhakikisha hakuna mtumishi hewa atakayebainika kwenye idara zao.

Katika utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilotoa Machi 15 mwaka huu kwa wakuu wa mikoa kufuatilia na kubaini watumishi hewa, Mkoa wa Dar es Salaam umebainika kuwa na watumishi hewa 209 walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni mbili.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Makonda alisema hayupo tayari kuendelea kuona watumishi hewa wanaendelea kuwapo. 

Alisema ni jukumu la kila mkuu wa idara kuhakikisha anasimamia eneo lake. Makonda alisema mkataba utaanza kazi rasmi baada ya siku saba.

Alisema baada ya hapo, atakayebainika kuwa na mtumishi hewa, atawajibika katika kulipa gharama zote za hasara alizoingiza kwa malipo yatakayofanyika.

“Nataka ndani ya siku saba hizi mpitie upya, mhakiki watumishi wenu baada ya hapo sitataka kusikia sababu yoyote lazima tufanye kazi kila mmoja kwa nafasi yake na msisubiri kila kitu msimamiwe,” alisema Makonda.

Pia aliwataka wakuu hao kuhakikisha kila mwisho wa wiki wanampelekea taarifa ya kila idara jinsi watakavyofanya kazi.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top