Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi Sophia Mjema ameongoza maandamano ya amani yaliyowashirikisha mamia ya makundi ya vijana Wakiwemo wajasiriamali,vijana walioacha kutumia madawa ya kulevya na kufanya matukio hatarishi na kuwataka vijana Kuachana na vitendo vya uhalifu badala yake wafanye kazi kwa bidii katika kuunga mkono jitihada za kutekeleza agizo la Rais Magufuli kuhamasisha vijana kufanya kazi nchi nzima.
Maandamano hayo yenye kauli mbiu Temeke ya Mjema “KIJANA ACHA ULEVI NA MADAWA YA KULEVYA FANYA KAZI WEKA TEMEKE SAFI” yameanzia babarabara ya uwanja Taifa kupitia Mandela uhasibu Mtoni kwa Azizi Ali na kufikia tamati katika viwanja vya Temeke mwisho jijini Dar es Salaam ambapo akizungumza na makundi hayo mkuu huyo amesema ni lazima Temeke uhalifu uishe kwa kufanya kazi.
Akitoa ujumbe kwa vijana juu ya athari za matumizi ya madawa ya kulevya kwa niaba ya vijana walioacha kutumia dawa hizo Aliwataka vijana wenzake kuacha imani potofu kuwa ukitumia dawa za kulevya ndio starehe pekee duniani.
Akizungumzia hali ya usafi ndani ya manispaa hiyo Afisa afya wilaya ya Temeke Bw.William Muhemu pamoja na kuitaka jamii kila mmoja kushiriki katika usafi bila kulazimishwa amesema kero ya harufu mbaya
Iliyokuwa ikilalamikiwa na wananchi katika vizimba vya kukusanyia taka Temeke mwisho na Mwembeyanga imefanyiwa Kazi.
Tayari serikali wilayani Temeke imetenga maeneo ya kufanyia kazi kwa vijana baada ya kubaini kuwa wengi wao hawana kazi ikiwemo eneo la masoko ambapo takribani wafanyabiashara 3890 watanufaika kwa kupatiwa mabanda katika maeneo tofauti likiwemo eneo katika kata ya Tuangama ambapo magari yatafika maeneo hayo sambamba na vijana kuwapa mikopo kutoka Taasisi za kibenki.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies