Hiki ndicho kilichofikiwa katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu Kahama.
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka jana iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Kahama mjini Bw.James Lembeli dhidi ya mgombea wa CCM Mh.Jumanne Kishimba imeendelea leo katika mahakama ya wilaya ya Kahama.
Kesi hiyo amnbayo iliendelea kuunguruma leo majira ya saa tano kamili huku wananchi waliofika mahakamani hapo kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo wakiilalamikia mahakama kutoweka vipaza sauti hali inayosababisha idadi kubwa ya wananchi waliofika kusikiliza kesi hiyo kushindwa kuelewa nini kinaendelea.
Aidha baada ya jaji Moses Mzuna kusikiliza hoja za kila upande na kuridhika na maelezo aliagiza pande zote mbili kuleta mashahidi wao ili waanze kutoa ushahidi na kuahirisha kesi hadi kesho siku ya jumatano tar.02/03 ambapo kesi itaendelea.