Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WILAYA YA MVOMERO KUWEKA MIPAKA YA MAENEO YA MASHAMBA NA MALISHO YA MIFUGO, KUJUA ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Wilaya ya Mvomero kuweka mipaka kutenganisha maeneo ya mashamba na malisho ya mifugo.

Halmashauri ya wilaya ya Mvomero inaanza kusafisha na kuweka mipaka ya barabara na mitaro kwa kila upande, kutenganisha maeneo ya ufugaji na yale ya mashamba katika vijiji vinavyozunguka bonde la Mgongolwa ili kukabiliana na migogoro na vurugu za mara kwa mara zinazojitokeza ambazo husababisha vifo vya watu na wanyama, uharibifu wa mali na majeruhi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero, George Mkindo, amesema hayo wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi, Mwigulu Nchemba, ukishirikisha vijiji vinavyozunguka na kulitumia bonde hilo ambapo amesema mipaka hiyo inatarajiwa kuanza kuwekwa mapema wiki hii na mkandarasi kutoka kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kwa kusafisha barabara yenye urefu wa kilometa 11 ikiwa na upana wa mita saba kwa kila upande kuzunguka eneo la mgogoro, na katikati yake utachimbwa mtaro ili mifugo isivuke upande wa malisho kwenda mashambani, huku mkuu wa wilaya ya Mvomero Betty Mkwasa akisema wameweka mipango ya muda mrefu na mfupi kukabiliana na migogoro.

Mbunge wa Mvomero Suleiman Sadiq amesema zoezi hilo litashirikisha na kuzingatia wataalam wa halmashauri wakiwemo wa ardhi, viongozi wa vijiji na kwamba kikosi kazi kutoka wizara ya ardhi nao wamefika wilayani humo kuanza upimaji na uwekaji mipaka, na kushauri jeshi la polisi kuimarisha ulinzi ili shughuli za maandalizi ya kilimo ziendelee huku akimuomba rais Dk John Magufuli kufuta hati miliki zidi ya mashamba pori waliyopendekeza, baada ya kufanikiwa kuyafutia umiliki mashamba saba kati ya 33 yaliyopendekezwa.

Waziri Nchemba aliyetaka jeshi la polisi kufanya doria za mara kwa mara katika maeneo hayo badala ya kusubiri tatizo kuwa kubwa, amewaeleza wananchi hao kuwa mipaka peke yake haitatosha kuondoa migogoro baina ya pande hizo mbili kama kila mmoja hataheshimu matumizi yake na kuzingatia utawala wa sheria, na kwa kila mmoja kutambua thamani ya shughuli anayofanya mwenzake huku akiwaonya kuacha kuishi kwa visasi, chuki na udanganyifu wa matukio.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top