Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WANANCHI WAVUNJA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI SHMBA LA MWEKEZAJI KILIMANJARO, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Wananchi wavunja miundombinu ya umwagiliaji shamba la mwekezaji TPC Kilimanjaro.

Wakulima wa mpunga katika skimu ya umwagiliaji Mawala kata ya Kahe wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamevamia na kuharibu miundombinu ya ugawaji maji kupeleka katika mashamba ya miwa ya  mwekezaji wa kiwanda cha sukari TPC.

Wakulima hao wamesema wamelazimika kufanya uharibifu huo na kuelekeza maji katika mfereji wa mashamba ya wakulima kwa madai ya mwekezaji huyo kukausha maji yote mferejini na kuelekeza kwenye mashamba ya miwa hali ambayo imesababisha kusababisha mpunga uliopandwa kukauka kwa kukosa maji.

Wamesema wanasikitishwa na hatua ya mwekezaji huyo kukiuka makubaliano ya kugawana maji hayo kwa wiki siku tatu badala yake anatumia mashine ya kuvuta maji yote mferejini na kueleleza kwenye mashamba ya miwa hali ambayo imesababisha mashamba ya mpunga kukauka kwa kukosa maji.

Diwani wa kata ya Kahe mashariki Bw. Rodrick Mmanyi amelazimika kufika katika eneo la tukio na kuwataka wakulima kuacha kufanya vurugu na kuahidi kushirikiana na viongozi wa umoja wa wakulima hao ili kufanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda cha sukari TPC kumaliza mgogoro huo ambao unahatarisha amani.

Hata hivyo juhudi za kumpata afisa utawala wa kiwanda cha sukari TPC Japhary Ally kuzungumzia mgogoro huo hazikufanikiwa baada ya kusema yuko kwenye kikao ambapo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Ramadhani Mungi amesema amepata taarifa hizo na kwamba yuko safarini atatoa taarifa hizo kesho.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top