Wahamiaji haramu 13 raia wa Ethiopia wamekamatwa mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Wahamiaji haramu 13 raia wa Ethiopia wamekamatwa katika kichaka eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania huku baadhi yao wakiwa na hali mbaya kiafya kwa madai ya kutembea katika kipindi cha mwezi mzima hadi kuingia nchini bila kula chakula cha uhakika.
Wahamiaji hao wamekamatwa na idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi kufuatia timu maalum iliyoundwa na watendaji wa serikali waliopo katika eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania kufuatia kuwepo kwa mtandao wa kusafirisha wahamiaji hao kuwapeleka Afrika ya Kusini.
Katika operesheni hiyo baadhi ya wakaguzi wa mamlaka ya chakula na dawa nchini tawi la Horohoro wameanza operesehni ya kukagua vyombo vyote vya usafiri ikiwemo magari ya abiria ili kubaini bidhaa zilizopitwa na muda wake kwa lengo la kunusuru afya za watanzania.