Na Malisa Godlisten,
Siku chache baada ya Mhe.John Pombe Magufuli kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuanza "kutumbua majipu" rafiki yangu mmoja ambaye ni mwandishi wa gazeti moja la kila siku aliniambia hii ni nguvu ya soda.
Alisema Magufuli anaweza kuwa na dhamiri ya kweli ya kufanya mabadiliko lakini atakwamishwa na chama chake. Bado chama chake hakijawa na dhamira ya kweli ya kutaka mabadiliko. Hata majipu anayotumbua kuna mengine hayatumbuliki maana yanagusa uhai wa chama chake.
Aliifananisha dhana ya "kutumbua majipu" na "kuvua gamba" ambayo ilitumika na chama cha mapinduzi miaka kadhaa iliyopita kama ajenda ya kupiga vita ufisadi. Lakini ajenda hii ilishindwa kuvua hata gamba moja ndani ya chama hicho licha ya kupigiwa chapuo na viongozi wakuu wa chama hicho.
Kwahiyo dhana ya "utumbuaji wa majipu" ni sawa na "uvuaji gamba". Kuna majipu hayawezi kutumbulika hata kama Rais Magufuli ana dhamira ya kufanya hivyo.
Moja ya jipu kubwa kabisa ambalo lipo usoni kwa Magufuli na amelikalia kimya kama hajaliona ni suala la umeya wa Jiji la Dar es Salaam. Hili ni jipu ambalo Magufuli ameshindwa kulitumbua na haoneshi kuwa na mpango huo.
Tangu uchaguzi mkuu ufanyike na wananchi kuchagua wabunge na madiwani yapata miezi minne sasa. Katika kipindi hiki cha miezi minne jiji la Dar es salaam ni kama limesimama.
Jiji halina Meya, hakuna kamati za halmashauri, hakuna mipango ya maendeleo, hakuna vikao vya madiwani, jiji limesimama kwa sababu ya mvutano wa kisiasa kati ya CCM na Muungano wa vyama vya UKAWA juu ya nafasi ya Umeya.
Mvutano huu umesababishwa na CCM kutokubali kuachia madaraka ya kuongoza jiji la Dar kwa vyama vya upinzani. Bado haijajulikana hofu ya CCM inatokana na nini lakini hadi sasa wamefanya mbinu mbalimbali kuhakikisha wanahujumu uchaguzi wa Umeya wa Dar na kuweza kuongoza tena jiji hili.
Baadhi ya mbinu zilizotumika ni pamoja na kutumia wabunge wa viti maalumu kutoka Zanzibar ambao baada ya mvutano mkubwa wa kisheria walizuiwa kupiga kura ya kumchagua Meya.
Lakini watu wanahoji kwanini CCM walete wabunge wa Zanzibar kuja kupiga kura Dar? CCM walijua kuwa wabunge wa Zanzibar hawana uhalali wa kisheria wa kupiga kura bara lakini wakalazimisha. Kwanini? Endelea na habari hii kwa {{KUBONYEZA HAPA}}
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies