Featured

    Featured Posts

Loading...

TFDA YAKIFUNGIA KIWANDA BAADA YA KUGUNDUA KINATUMIA MALIGHAFI ZENYE SUMU, ZAIDI BOFYA HAPA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) imekifungia kwa muda usiojulikana kiwanda cha kukamua mafuta yanayotokana na mbegu za pamba cha Yobama Shirecu kilichopo kata ya Lugulu wilayani Itilima kutokana na kutumia malighafi zenye sumu.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa zaidi ya magunia 600 ya mbegu zisizofaa yamegundulika , huku lita 520 za mafuta zikifikishwa polisi kama ushahidi.

Akiongea baada ya kukagua uzalishaji wa mafuta na kufikia uamuzi wa kukifungia kiwanda hicho Mkaguzi mwandamizi TFDA kanda ya Ziwa Julius Panga amesema kuwa wamefunga kiwanda hicho kutokana na kutumia mbegu zenye sumu ambazo ziliandaliwa kwa ajili ya msimu wa kilimo na siyo kukamua mafuta.

Panga amesema kuwa malighafi inayotumia kutayarishia mafuta katika kiwanda hicho haikidhi ubora na usalama, ambapo mbegu zina dawa kwa ajili ya kupandwa shambani pia mazingira ya kiwanda hicho si rafiki kwa mlaji wa bidhaa hiyo.

Aidha mkaguzi huyo ametoa wito kwa wanunuzi na walaji kuhakikisha wanaangalia muda wa kuisha matumizi ya bidhaa na pindi wanapobaini ni vema wakatoa taarifa kwa mamlaka husika.

Kwa upande wake afisa usafi na mazingira wilaya ya Itilima Kelisa Wambura amesema ameunga mkono hatua zilizochukuliwa na TFDA na kuahidi kusimamia agizo hilo.

Naye afisa afya wa mkoa wa Simiyu, Makoye Madaraka amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kubaini viwanda bubu ili kuhakikisha wote wanaotengeneza chakula kwa malighafi ambayo ni hatarishi wanachukuliwa hatua sitahiki.

Jumla ya dumu 52 za lita kumi kumi za kuhifadhiwa mafuta zilikamatwa na kupelekwa polisi kwa uchunguzi zaidi.

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top