Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

SERIKALI YA TOA SIKU 14 KWA BODI YA DAWA MSD ARUSHA

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Serikali yaitaka bodi ya dawa MSD kusafisha wezi wa dawa mkoani Arusha.

Serikali imetoa siku 14 kwa mkurugenzi mkuu wa bodi ya dawa kuhakikisha watendaji wote wanaotajwa kuhusika na mtandao wa wizi  wa dawa na walioshindwa kuchukua hatua wanawajibishwa kabla hatua kubwa zaidi hazijachukuliwa.

Akizungumza wakati anazindua duka la MSD kanda ya kaskazini lililopo katika hosipitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru naibu waziri wa afya Dr. Hamisi Kigwangala amesema ni jambo lililoko wazi na lisilo na shaka kuwa ubadhirifu upo na wahusika wapo hivyo ni bora  yaliyoko ndani ya bodi yakafanyika kwani hakuna njia ya mkato.

Aidha Dr Kigwangala amesema kimsingi MSD inajitahidi kufikisha dawa kwa walaji lakini jitihada hizo haziwezi kuwa na tija kama baadhi ya watendaji wezi na wasiowajibika wataendelea kupewa nafasi na amefafanua na amewataka wasimamia dawa za serikali wakati serikali ikiendelea kuhakikisha kuwa dawa zinakuwa na nembo.

Akizungumza baada ya kufunguliwa kwa duka hilo lililogharimu milioni 47 mkurugenzi mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu, amesema kazi ya kukabiliana na wizi wa dawa, kuchukua hatua kwa wanaohusika inaendelea sambamba na kufungua maduka ya dawa kwenye mingine ukiwemo wa Mbeya.

Duka hilo lililofunguliwa Arusha litakuwa likihudumia mikoa ya kanda ya kaskazini ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara zenye vituo vya afya 919, zahanati 852. Hospitali maalum, na hospitali za rufaa.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top