Jeshi la Polisi limeagiza maaskari nchi nzima kufanya operesheni maalum ya kuwakamata madereva bodaboda na abiria wanaukubali kupanda zaidi ya wawili-maarufu mishikaki- na wanaopita katikati ya magari na kuwasweka rumande kabla ya kuwafungulia mashtaka ya kuvunja sheria ya usalama barabarani.
Akitoa agizo mbele ya waandisihi wa habari, msemaji wa jeshi la Polisi makao makuu ya Polisi SSP Advera Bulimba amesema opereshani hiyo itaenda sambamba na kuwakamata madereva bodaboda wanaohatarisha maisha ya wananchi na vyombo vya usafiri kwa kupita katikatio ya magari, pamoja na madereva walevi.
Kuhusi siku kuu ya Maulid, X-mas na mwaka mpya, amesema jeshi la Polisi limewataka wananchi kutoa taarifa mapema iwapo wanaona sura ya watu wasioeleweka katika maeneo yao.
Pamoja na viashiria vingine vya uvunjifu wa amani ili ziweze kuchukuliwa hatua za haraka ambapo amewataka wamiliki wa kumbi za starehe kutojaza watu kupita kiasi.
Pia ikumbukwe kwamba magari yote nchini yamepigwa marufuku kubeba abiria zaidi ya level seat, na wameongeza kwamba gari litakarokamatwa sheria itawachukulia hatua dreva pamoja na abilia wote watakaokuwa wamezidi.