HABARILEO. Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa
Halmashauri nchini wametakiwa kuhakikisha takataka zote zilizolundikwa
wakati wa kazi ya usafi iliyofanyika Desemba 9, nchini kote
zinaondolewa.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George
Simbachawene wakati akizungumza na watumishi wa wizara hiyo mjini hapa,
na kuagiza kuwa ifikapo Desemba 20, mwaka huu takataka zote
zilizolundikwa ziwe zimeondolewa.
“Naagiza wakuu wa mkoa, wilaya na
wakurugenzi kuwa ifikapo tarehe 20 mwezi huu takataka zote ziwe
zimeondolewa katika maeneo yao,” alisema Simbachawene na kuongeza kuwa
hategemei kusikia baada ya tarehe hiyo takataka kuwa bado zimelundikana
kwenye maeneo mbalimbali.
Kumekuwapo na mlundikano wa takataka
katika maeneo mbalimbali ya miji nchini na kuwa uchafu baada ya kazi ya
usafi ya Desemba 9, nchini kote kutokana na agizo la Rais John Magufuli
la kufuta sherehe za sikukuu ya Uhuru na badala yake siku hiyo itumiwe
kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies