Rais John Pombe Magufuli anaendelea kutimiza ahadi yake ya kuleta mabadiliko Tanzania kama alivyoahidi, akichukua hatua za kupambana na ufisadi na kuhakikisha kuna uwajibikaji serikalini.
Miongoni mwa hatua za karibuni ni pamoja na kumuondoa kwenye wadhifa wake Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU Dr Edward Hoseah aliyeteuliwa na rais wa zamani Jakaya Kikwete mwaka 2006 pamoja na maafisa wengine wanne.
Magufuli anasisistiza anataka maafisa watakaoendana na kasi yake, kwa kuzingatia kauli yake mbiu "Hapa kazi tu." Mpaka sasa amepata uungaji mkono wa viongozi wa upinzani na sehemu kubwa umma.
Swali ni jee atafanikiwa? Tume maoni yako