Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

UWENDA HIKI NDICHO CHANZO CHA ZANZIBAR KUFUTIWA MATOKEO?

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Oktoba 25, 2015 ndio ilikuwa siku ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchi nzima yaani Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

Lakini siku ya Oktoba 28 wakati watanzania wakiendelea kupokea matokeo ya uchaguzi huo watanzania walifikiwa na taarifa mpya kutoka Zanzibar kuhusu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha kutangaza kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi huo kwa upande wa Zanzibar !!

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alizitaja sababu za tume hiyo kufikia uamuzi wa kufuta matokeo hayo ambapoa alisema “Baadhi ya Wajumbe badala ya kuwa Makamishna wa Tume, wamekuwa wawakilishi wa vyama vyao".

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar,  Jecha Salim Jecha.

Aidha Jecha alisema sababu nyingine ya kufuta matokeo hayo ni kumegundulika kasoro nyingi katika Uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kugundulika kwa baadhi ya vituo vimekuwa na kura nyingi zaidi kuliko daftari wa wapiga Kura.

Mwenyekiti huyo pia aliainisha kwamba taarifa iliyowasilishwa na Wajumbe wetu waliowakilisha Tume Pemba, kulifanyika uhamishaji wa masanduku ya kupigia Kura na kuhesabiwa kwenye maeneo nje ya vituo vya kupigia kura kinyume na taratibu.

“Kuna vijana walivamia vituo na kufanya fujo kuzuia watu na kuzuia wengine kupiga Kura… Kuna vyama vya Siasa viliingilia majukumu ya Tume na kujitangazia ushindi na kupeleka mashinikizo kwa Tume… pia kulikuwa na malalamiko ya vyama mbalimbali kutoridhika na mchakato wa kupiga Kura, kuhesabu na matokeo.” alisema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha.

Pamoja na hayo, Mwenyekiti huyo alisema “Kuna namba za Fomu za matokeo zilionekana kufutwa na kuandikwa upya namba nyingine juu yake, hivyo kufuatia sababu zote hizo  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha alisema  kwa kuzingatia hayo, nimeridhika kwamba Uchaguzi haukuwa wa haki na kumekiukwa sheria na taratibu za uchaguzi… Natangaza Uchaguzi huu na matokeo yake umefutwa, kuna haja ya kufanyika uchaguzi mwingine." 
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top