Taasisi ya sekta binafsi nchini - TPSF imewaomba wananchi na wadau
wengine kwa ujumla kudumisha amani na utulivu wakati na baada ya
uchaguzi mkuu ili Tanzania iendelee kuwa na mazingira mazuri ya kufanya
biashara na uwekezaji.
Akitoa tamko la sekta binafsi kwa waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania -TPSF
Bw. Godfrey Simbeye amesema biashara na uwekezaji ni nguzo muhimu za
kujenga uchumi na kukuza pato la taifa litakaloiwezesha Tanzania kuwa
nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Bw.Simbeye pia amevitaka vyombo vitaka vyosimamia uchaguzi mkuu
kutenda haki kwa mujibu wa sheria, na kuwataka wananchi kuzingatia
sheria na maelekezo yatakayotolewa na serikali.
Mkurugenzi huyo mtendaji amesema sekta binafsi imelazimika kutoa
tamko hilo baada ya baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji kupenda
kuhakikishiwa uwepo wa amani na utulivu ili waweze kuendelea na biashara
zao.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies