Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

TAARIFA ZA MWANZO KABLA YA VIFO VYAO

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Usiku wa kuamkia leo October 16 2015 majukwaa  ya siasa Tanzania yametawaliwa na ajali ya Helikopta ambayo imeanguka na kulipuka kwenye mbuga ya Wanyama ya Selous ambapo Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alithibitisha kwamba mmoja wa waliokuwemo ndani ni Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).

Kupitia  ukurasa  wake  wa  Twitter,Nyalandu  aliandika;
"Tumetuma vikosi vya maafisa na maaskari katika eneo la Selous kulikotokea ajali ya helikopta katika harakati za uokozi, ajali ya helikopta imetokea katika kitalu R3 ndani ya mbuga ya Selous na mashuhuda wanasema ilianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha

"Mashuhuda wa ajali ya helikopta iliyotokea Selous walikuwa kitalu R2 na walishuhudia ikianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha Kitalu R3, Maafisa na Maaskari wanaelekea eneo la tukio kutokea Msolwa na Matambwe na tumeagiza vikosi vilivyo kwenye doria Selous kushiriki uokoaji

"Mashuhuda wa ajali ya helikopta Selous walikuwa Kitalu R2 wanasema ilianguka baada ya majira ya saa 12 jioni na kulipuka, serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii inachukua hatua zote kuwafikia wahanga na majeruhi wa ajali ya helikopta Selous usiku huu

"Nimeagiza section 2 zenye askari 16 kutoka Matambwe na Msolwa (Selous) kwenda eneo la tukio, RPC Morogoro na mkuu kanda ya Msolwa (Selous) wanashirikiana, hatujui kitakachokuwa kimewapata wasafiri ndani ya helikopta iliyoanguka akiwepo Mh, Filikunjombe, tuungane kuwaombea kwa Mungu"

Katika taarifa nyingine kutoka upande wa CCM iliyotolewa na naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia January Makamba mida ya saa sita usiku ilisema:  "Tumesikia habari za chopa kuanguka huko Selous. Mungu aepushe kusiwe na majeruhi. Chopa zote zinazotumiwa na CCM kwenye kampeni ziko salama"

Baadae aliandika :"Kwakuwa ilisemekana kuwa chopa ya kampeni ya CCM imeanguka, tulifuatilia/kubaini/kuripoti kuwa tulizokodi kama Chama hakuna iliyoanguka". Hiyo ndio ilikua tweet ya mwisho kuandikwa na January Makamba usiku lakini badae aliretweet kilichoandikwa na Waziri Nyalandu na Zitto Kabwe.

Zitto aliandika: "Naomba utulivu.(1) ajali ya helkopta imethibitishwa (2) kuwaka hakujathibitishwa (3) ndugu yangu Deo alikuwamo (4) hakuna uthibitisho wa madhara, naomba utulivu mpaka tupate taarifa rasmi zilizothibitishwa na mamlaka husika, naomba sana hilo ili kuepuka sintofahamu"

HELIKOPTA YA CCM YAANGUKA NA KUUWA WATU WOTE, CLICK HERE

Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top