Featured

    Featured Posts

Loading...

KLABU YA MAJIMAJI YA MJINI SONGEA YAMTIMUA KATIBU WAKE MKUU

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.

Na Andrew Mhaiki, Songea KLABU ya Majimaji ya Songea imemtimua kibarua Katibu wake Mkuu , Zacharia Ngalimanayo kwa kile kilichodaiwa kughushi saini za wajumbe kinyume na taratibu za kisheria za klabu hiyo na kwenda kuchukua fedha benki kiasi cha Sh 200,000 kwa matumizi yake binafsi.

Akizungumza na gazeti hili jana , Mwenyekiti wa Wanalizombe hao, Humphrey Milanzi alisema kuwa hatua ya kumtimua kibarua katibu huyo , Ngalimanayo ilifikiwa katika kikao cha pamoja na uongozi wa Bodi ya klabu hiyo baada kujilidhisha kwa kupata ukweli kutoka kwa maofisa wa benki ya CRDB tawi la Songea.
Alisema kiasi hicho cha fedha ambacho alichokichota ni kati ya fedha zilizotolewa na wahisani kwa ajili ya kuiwezesha klabu hiyo kusaka wachezaji na kuwasajili kwa ajili ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.


Alisema Majimaji ni klabu ambayo inajiendesha kupitia michango ya wanachama na fedha za wahisani katika kufanikisha maendeleo yake ya soka, ambapo kwa sheria ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) kwa nafasi ya Katibu Mkuu na Meneja anakuwa waajiliwa , ambao wanaajiliwa na klabu hiyo na kulipwa mshahara tofauti viongozi wengine wanafanyakazi kwa kujitolewa kuongoza klabu hiyo.

Alisema uongozi wa Bodi ya klabu hiyo imechukua hatua hiyo ya kumtimua kwenye uongozi pamoja na kumtaka arejeshe haraka fedha hiyo ili iweze kutumika kama ilivyokusudiwa ili waendelee kujenga imani kwa wanachama wao pamoja na wahisani katika kipindi hiki kigumu cha usajili wa wachezaji kwa kumpa muda wa mwezi mmoja kurejesha kiasi hicho cha fedha Sh 200,000 ambazo alizichota kutoka kwenye akaunti ya klabu hiyo.

Hata hivyo katika kuthibitisha hilo , Ngalimanayo hakuweza kupatikana pamoja na kumpigia kwenye simu yake ya kiganjani yenye namba 0752-622887 ilikuwa haipo hewani kwa muda wote ilikuwa imefungwa, kitu ambacho kilibainika suala hilo la kujichotea fedha benki kinyume cha sheria kwa kughushi saini za wajumbe lililofanywa na Katibu huyo lilikuwa na ukweli.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top