Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

HUAWEI KUFANYA KONGAMANO LA SEKTA YA TEKNOLOJIA IT

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Tarehe 18 na 19 Juni 2015, ndani ya ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) uliopo mkoani Dar es Salaam, kampuni ya Huawei Tanzania itashirikiana na Wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kufanya kongamano la sekta ya Teknolojia ya IT. Kongamano hili litazungumzia teknolojia mpya ya IT ikiipa kipaumbele sekta mpya ya kuhifadhi data kwa kutumia njia ya mawingu/cloud storage.

Lengo na dhumuni ya kongamano hili ni kuendelea kuwawezesha Watanzania kwa njia moja au nyingine kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. kila mmoja wetu anaelewa kua kwenye karne hii ya mawasiliano; teknolojia ya habari na mawasiliano ni muhimu sana hususani katika shughuli zetu za kila siku ziwe za kibinafsi au za kibiashara
Kwa kupitia teknolojia ya Habati na Mawasiliano, dunia inakua connected zaid na zaid huku viwanda vilivyopo vikihitaji revamp kuhakikisha biashara inaendeshwa efficiently and sustainability.

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imewezesha kwa kiasi kikubwa ukuaji wa sekta mbalimbali na kufanya ongezeko la uvumbuzi wa vitu mbalimbali na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mahitaji ya employment hususani kwa upande wa vijana Huawei Technologies Tanzania co. Ltd, imekua katika kiini cha mzunguko wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ulimwenguni ; ikiendesha shughuli zake katika kila nchi mbalimbali duniani. Huawei imejizatiti huku kuhakikisha kua kiongozi kwenye uvumbuzi wa teknolojia mpya pamoja na ukuaji na ongezeko la maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo, viwanda, biashara, n.k

Kampuni ya Huawei Tanzania imewekeza nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa na has commited zaidi kwenye ukuaji wa maendeleo ya sekta ya Habari na Mawasiliano nchini. Katika sekta hii ya Habari na Mawasiliano, kampuni ya Huawei Tanzania imelenga Zaidi kwenye upande wa elimu na mawasiliano na imeahidi kuendelea kufanya hivo.
Mwaka 1998, Kampuni ya Huawei Tanzania ilianza shughuli zake nchini Tanzania na mpaka hadi leo ina wafanyakazi Zaidi ya 315 kupelekea kufanya idadi ya watanzania kua na Zaidi ya asilimia 75. Toka ianze shughuli zake za kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, Kampuni ya Huawei Tanzania imekua ikishikiriana na wadau wengine mbalimbali wa ICT ikiwemo mashirika binafsi, mashirika ya uma pamoja na Serikali ya Tanzania.

Kampuni ya Huawei Tanzania inaongoza katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania na imekua ikishirikiana na wadau wengine wa mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel na TTCL katika kuchangia ukuaji wa individuals kwenye hii sekta (ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top