Kampeni ya zuia ajali sasa yazinduliwa, ambapo abiria watakiwa kutoa taarifa kwa kutumia namba maalum ili kuzuia mwendo kazi wa magari/mabasi yaendayo mikoani pamoja na kupunguza vifo vya abiria.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani bwana Mohamed Mpinga ndiye alikuwa msemaji mkuu katika uzinduzi wa kampeni hii ya zuia ajali akishirikiana na Deogratius Rweyunga mkurugenzi wa radio one pamoja na Bi. Rosalyin Mworia ambaye huyu ni mkuu wa Mawasiliano Vodacom Tanzania.
Katika kampeni hii namba itakayotumiwa na abiria kutoa taarifa police juu ya gari ambalo linatembea kwa mwendokasi kinyume na matakwa ya abiria itakuwa ni 0800 757 575 Huduma hii ni kwa watumiaji wa simu mitandao yote, ambapo wewe abiria utatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya sms kwenda namba hiyo tajwa hapo juu.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies