Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Serikali imekataa mapendekezo ya bajeti ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa shilingi bilioni 10, Raia Mwema limeambiwa.
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ambayo CAG ndiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wake ilikuwa imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 86 katika bajeti yake ya mwaka huu wa fedha (2015/2016) lakini sasa itapewa shilingi bilioni 76 tu.
Makato haya ni ya kihistoria kwa vile kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008, serikali haitakiwi kukata bajeti hiyo wakati ikiwa tayari imepitishwa kupitia utaratibu wake. Kwa maneno mengine, serikali imekiuka sheria katika suala hili.
Kwa mujibu wa mapendekezo ya kibajeti ambayo gazeti hili limeyaona, ofisi hiyo ambayo bajeti yake inasomwa pamoja na ile ya Wizara ya Fedha, itakuwa na upungufu wa asilimia 12 ya kiwango kilichotakiwa.
Kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, bajeti ya CAG hupangwa katika kikao maalumu baina ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Wizara ya Fedha na CAG.
Sheria hiyo inaeleza kwamba endapo bajeti itapitishwa kwenye kikao hicho, kwa kiwango chochote kile, inabidi serikali itoe kiasi hicho kama kilivyotakiwa bila kupunguza.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Bariadi Mashariki na Mwenyekiti wa chama cha United Democratic (UDP), John Cheyo, utaratibu huo umewekwa ili kuhakikisha kwamba ofisi hiyo inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
“CAG anatakiwa aandae bajeti yake na kisha awasilishe mapendekezo yake. Baada ya mapendekezo hayo kujadiliwa katika kikao hicho, bajeti hupitishwa. Kiwango hicho hakitakiwi kupunguzwa kwa sababu kwenye kikao kuna Bunge na Serikali na ndiyo maana ya uwepo wao,” alisema Cheyo ambaye ni miongoni mwa wabunge wa Afrika wenye uelewa mkubwa wa masuala ya uwajibikaji.
Akizungumza na Raia Mwema kuhusu taarifa hizi za kupunguzwa kwa bajeti, Mwenyekiti mstaafu wa PAC, Zitto Kabwe, alisema katika kikao cha mwisho cha mapitio ya bajeti ya CAG, kiwango kilichopitishwa kilikuwa ni shilingi bilioni 86.
“Unasema wamepunguza zaidi kiwango? Basi watakuwa watu wa ajabu sana. Hii ni kwa sababu, mahitaji ya kibajeti ya CAG yalikuwa shilingi bilioni 94 lakini serikali ilijieleza kwamba ina hali ngumu na isingeweza kutoa kiasi hicho.
“Ndiyo tukakaa tena chini na kukubaliana kuhusu kiasi hicho cha shilingi bilioni 86. Sasa kama na hiyo wamepunguza tena basi hapo kuna tatizo. Hebu cheki ujue kama labda kuna kikao kimefanyika kati ya CAG, PAC na serikali kuhusu jambo hilo,” alisema Zitto ambaye sasa ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo.
Mmoja wa wajumbe wa PAC, Ismail Aden Rage, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini (CCM), alilithibitishia gazeti hili kwamba hakuna kikao kilichokaa kupunguza bajeti hiyo ya PAC. Juhudi za kumpata Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, kuzungumzia kuhusu suala hili hakifanikiwa kwa vile inaelezwa yuko nje ya nchi kikazi.
Gazeti hili limeambiwa kwamba hatua hii ya serikali inaweza kuwa na athari kubwa kwenye ofisi ya CAG kwa vile mwaka huu inatarajiwa kufanya kaguzi maalumu kwenye maeneo ya gesi na mafuta.
CAG imeamua kuingia katika eneo hilo la gesi na mafuta kwa lengo la kulisaidia taifa kubaini endapo mikataba ambayo nchi imeingia kwa sasa itakuwa na faida au la katika miaka ijayo.
CAG pia imeongeza mawanda yake ya ukaguzi kwa kukagua pia misamaha ya kodi na maeneo mengine kama vile bidhaa zinazodaiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi lakini zikipitia hapa nchini; mambo yote hayo yakihikitaji ongezeko la fedha.
Powerd by Raia Mwema.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.
Share habari hii kadri uwezavyo.