Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Mwaka juzi kulikuwa na sintofahamu kuhusu nani achinje iliyosababisha kifo cha mchungaji moja kanda ya ziwa. Wakati sarakasi hiyo ikiwachanganya watanzania, katibu wa Bunge Thomas Kashillah aliibuka na kusema, Bunge halitaoneshwa tena kwenye Runinga nchini.
Mjadala ukahama kutoka uchinjaji na kuwa Bunge kutooneshwa. Serikali ikafanikiwa, kombe likafunikwa na mwanaharamu akapita.
Mwaka 2013 mvua kubwa kuliko hii ya mwaka huu ilinyesha na kusababisha mamia ya watu kulala njiani na njaa wakiwa na watoto wao.
Njia nyingi za kuingia katikati ya mji wa Dar zilifungwa na maji na matokeo yake watu wakawa na hasira na serikali kutosimamia miundo mbinu vizuri jambo lililosababishia wao kupata madhara yale.
wakati hayo yakipamba kwenye vyombo vya habari ghafla tukaambiwa Makamu wa Rais, waziri magufuli na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam wameanguka na helikopta. kama kwaida Mjadala ukahama kwa walioanguka na helikopta.
Mwanaharamu akapita tena, Ikumbukwe kuwa hakuna kati ya wote walioanguka na helikopta aliyeenda hospitali wala picha ya helikopta iliyoanguka haikuonekana mpaka leo kama kaburi la Daudi Balali wa EPA iliyoibuliwa na Dr Slaa.
Wakati wa Bunge la katiba, Tundu Lissu na UKAWA waliibua madudu mengi kuhusu muungano hasa pale walipohoji lilipo kaburi la waasisi wa muungano amabao ni Hanga na wenzake.
Wakati mjadala huo ukishika kasi Dodoma, ghafla serikali ikaibuka na ugonjwa wa Dengue. Tukaambiwa wamekufa watu wawili mara watatu wakati malaria inaua zaidi ya watu watatu kila siku achilia mbali hao watatu hata kama ni zaidi ya watatu waliokufa mara moja na Dengue. Baada ya hoja ya Muungano kupita Dengue nayo ikayeyuka bila maelezo ya kutosha.
Je, watu wameshajiuliza kwanini magaidi feki wa amaboni walikuja wakati hoja ya ESCROW ikivuma? Tuliambiwa kuna askari wetu wamekufa. Je, akina nani kwa majina na walizikwa wapi na lini? Nani ameona picha hata moja ya askari wetu?
Mifano ya usanii huu wa serikali kuibua hoja ili kujilinda au kufunika udhaifu wake ni mingi sana.
Huko nyuma nilishaandika zaidi ya mifano kumi ya namna hii. Mifano hii michache inatosha kujenga hoja yangu. Kwa nini nimeyaeleza yote hayo?? Sababu ni moja tu ambayo ni kama ifuatavyo hapo chini.
Jana jioni nilimsikia kwenye ITV mwenyekiti wa MOAT ndugu Reginald Mengi akilalamikia serikali kutaka kupeleka mswada wa uhuru wa habari ambao moja ya kipengele chake kinavilazimisha vyombo vyote vya habari vikiwepo ITV, STAR TV, Chanel ten nk vijiunge na TBC saa mbili usiku kwa taarifa ya habari.
kwamba vyombo vingine (TV zingine/zote) havipaswi kuwa na taarifa yao ya habari wenyewe badala yake sheria itawalazimisha wajiunge na TBC. Je, hili linawezekana??
Mimi Nina wasi wasi nalo. Siamini kabisa nikirejea mifano tajwa hapo juu. Kwa maoni yangu taarifa hii imeletwa ili kubadilisha au kusahaulisha au kufunika mjadala wa ufisadi wa zaidi ya trilioni moja ulioibuliwa na Chadema baada ya kuchambua ripoti ya CAG.
Kwa hiyo, taarifa hii imeletwa makusudi wakati bunge na vyombo vya habari vikijadili ufisadi huu wa serikali. Nijuavyo, Bungeni wakishamaliza taarifa hii ya TV zote kujiunga na TBC saa mbili jioni nayo itakuwa kama taarifa ya Dengue, hoja ya kashilillah ya Bunge kutooneshwa na TV au helikopta kuanguka bila majeruhi wala picha yake kuonekana.
Kama kicha cha habari hii kinavyosema "ni haki yangu kisheria kupata au kutoa habari" kwaiyo hoja hii ya kutunyima uhuru wa habari mimi siiungi mkono hata kidogo, maana iko kinyume na matakwa ya Watanzania na inakiuka haki za binadamu mpaka sasa.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.
Share habari hii kadri uwezavyo.