Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WANAJESHI ZAIDI YA 300 WAANDAMANA KISA AJIRA JESHINI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
VIJANA zaidi ya 300 waliopata mafunzo kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wameandamana kwenda Ikulu kumwona Rais Jakaya Kikwete ili asikilize kilio chao na kupinga upendeleo wa ajira ndani ya jeshi.

Maandamano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana kwa saa mbili asubuhi kwa vijana hao kujikusanya katika eneo la Jangwani huku wakiwa wameshika bendera nyekundu kupita barabara ya Morogoro, Umoja wa Mataifa hadi Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Vijana hao baada ya kufikia katika eneo hilo walizuiwa na askari polisi waliokuwa wameweka ulinzi maalumu huku wakiwataka kueleza matatizo yao kwani si kila jambo linapaswa kufanywa maandamano, mengine yanaweza kuzungumzwa.


Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Magesa Masatu, alisema lengo la maandamano hayo ni kupeleka kilio chao kwa Rais Kikwete baada ya kukosa ajira kwa muda mrefu ndani ya jeshi.
Alisema walifikia uamuzi huo baada ya kupeleka barua za maombi ya kazi Wizara ya Kazi na Ajira, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ulinzi bila kupatiwa ufumbuzi wowote.

“Vijana wengi wamekuwa wakipelekwa JKT na kuahidiwa kupatiwa ajira, lakini toka mwaka 2000 hadi 2014 wameajiriwa vijana wachache na wengine tumekuwa tukiachwa. “Kama Serikali haina uwezo wa kuajiri vijana kwanini wanatupeleka JKT na kutupatia mafunzo ambayo wanajua kuwa baadaye tunaweza tukayatumia vibaya kutokana tatizo la ukosefu wa ajira?

“Wengi hatuna kazi tunaishia kuzurura mitaani bila kazi yoyote, kutokana na hali hii mafunzo tuliyopewa yanaweza yakasababisha vijana wengi kufanya mambo ambayo baadaye yataleta adhari kwa taifa,” alisema Masatu.

Kwa upande wake Fabian Mashauri alisema wasipopata majibu mazuri kutoka kwa Rais Kikwete wataendelea kupigania haki yao hadi pale itakapopatikana. Pia alisema Serikali isipoangalia suala hilo la vijana, watakuwa wanatengeneza makundi hatarishi ambayo yatakuja kuliathiri taifa.


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    
In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top