Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WATU WA 4 WAUWAWA NA WENGINE 8 WAJERUHIWA ISRAEL

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Takriban waisreli wanne wameuawa na wengine 8 kujeruhiwa katika kile polisi wanasema ni shambulio la kigaidi dhidi ya Sinagogi eneo la magharibi ya Jerusalem.

Polisi inasema wanaume waliojihami kwa visu na mapanga wanaoshukiwa kuwa Wapalestina ndio waliofanya mashambulizi hayo. Washambuliaji wawili wamepigwa risasi na kuuawa.Israel imekuwa katika hali ya tahadhari kuu baada ya mashambulio kadhaa na Wapalestina wakizozana na Waisraeli kuhusiana na eneo takatifu ambalo wamekuwa wakizozania.

Vyombo vya habari nchini Israel vinasema kuwa ufyatulianaji risasi ulitokea kati ya polisi na washambuliaji hao waliowasili katika eneo hilo pindi taharuki ilipozuka. Msemaji wa polisi alieleza kwamba eneo la mashambulizi lilizibwa na kwamba waliojeruhiwa wakiwemo waumini sita na polisi wawili, walipokea matibabu katika hospitali mjini Jerusalem.

Watu wengine wanne wanasemekana kuwa hali mahututi na kwamba mshambuliaji wa tatu huenda ametoroka. Hali ya wasiwasi imekuwa ikikumba mji huo katika wiki chache zilizopita huku kukitokea mashambulizi makali yaliyofanywa na wapiganaji wa kipalestina dhidi ya raia waliokuwa wanatembea mjini.

Pia kumekuwa na wasiwasi kuhusu mpango wa Israel kujenga makazi zaidi ya walowezi eneo la Mashariki mwa Jerusalem.
 


Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.

    

In order you follow me just click one of the Icon Button above.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top