Kwa taalifa nikwamba, hali inazidi kutishia amani kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kutokana na vitendo vya kinyama vinavyoendelea kufanyika mkoani humo.
Ambapo siku ya juzi mkazi mmoja wa kijiji cha Rubangula aliyetambulika kwa jina la Krifu Christopher, alikutwa amefariki dunia huku akiwa amekatwa shingo na kunyofolewa ulimi wake katika eneo la Rwambi ambalo liko mpakani mwa kijiji cha Kiziru na Kagondo, ambavyo vijiji hivi ndivyo vijiji vya kwanza kabisa ukitokea Bukoba mjini.
Chanzo cha tukio la kuuwawa kwa mr. Krifu bado hakijafaamika, ila tukio la kuuwawa kwake lilitokea siku ya juma tano mida ya saa moja na nusu usiku, na mazishi ya mwili wa marehemu yalifanyika siku ya alhamis kijijini kwao Rubangula.
Ikumbukwe kwamba ni baada ya wiki moja tu ambapo kuna mwanakijiji ametoka kuchinjwa na watu wasio julikana. Na siku ya kifo cha marehemu Krifu, ililipotiwa kuwa kuna mtu mwingine ambaye naye amekutwa amechinjwa maeneo ya Kashai bukoba mjini. Jamani Polisi pamoja na vyombo husika tunaomba msaada wa kuweza kuzuia janga hili kwa wakazi wa mkoa wa kagera kwa ujumla.
Kwa habari za Matukio Kitaifa, Kimataifa, Michezo na Burudani, Ungana nami kupitia Link zifuatazo hapo chini.